Posts

BOKO HARAM WASHAMBULIWA NA NYOKA WA AJABU NA NYUKI, WAKIMBIA PORINI

Image
Wanajeshi wa Boko Haram wanaofanya mashambulizi na kuua raia wasio na hatia huko Nigeria linaelezwa kuanza kukimbia msitu baada ya nyoka wenye sumu kali na nyuki kuwashambulia. Habari hizi zilielezwa na mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa na kuthibitisha kuwa ni mmoja wa member wa kundi la Boko Haram na alieleza kuwa hivi sasa kundi hilo limelazimika kuhama msitu na linaelekea maeneo ya mpaka wa Nigeria na Cameroon baada ya wanajeshi wake wa ngazi za juu kushambuliwa na nyoka na kupoteza maisha. Kumezuka hisia za kiimani kuwa Boko Haram wanaadhibiwa na mizimu ya watu waliokuwa waliowauwa kinyama.Jeshi la Nigeria limeshafanya juhudi za kuwaondoa msituni lakini imeshindwa na hadi sasa kundi hilo linawashikilia wasichana zaidi ya 260 na bado linaendelea kushambulia Nigeria kwa mabomu ya kutegwa.

Kutana na mtaalamu Rob Ferrel kutoka Rob the Original Barbershop San Antonio ambaye hunyoa wateja kwa taswira za wachezaji wawapendao

Image
Wakati mashindano ya Kombe la Dunia yakishika kasi nchini Brazil, kimetokea kituko cha aina yake hasa kwa mashabiki wa soka nchini Marekani ambapo Salon moja mjini San Antonio inatoa ofa ya kunyoa nywele kwa michoro ya wachezaji mbalimbali nyota wanaotamba katika fainali hizo.  Katika wiki za hivi karibuni Rob Ferrel, mmilikiwa wa Rob the Original Barbershop, aliwanya watu kwa picha ya sura za nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo, mlinda mlango wa Marekani Tim Howard na Guillermo Ochoa kama sehemu ya ubunifu wake wa kunyoa.  Licha ya timu ya Ronaldo kuondolewa kwenye hatua ya makundi, walinda mlango wa Marekani Howard na Mexico Ochoa watakuwepo kwenye hatua ya mtoano. Vipi kuhusu hii? Rob Ferrel akimnyoa mteja kwa sura ya mlinda mlango wa Marekani Tim Howard Amemaliza: Tim Howard na bendera ya Marekani Miaka minane iliyopita Ferrel alikuwa anafanya kazi kwenye barbershop moja mjini Texas wakati ambapo kijana huyo alipoa...

ANGALIA PICHA JINSI WANACHAMA WA SIMBA WALIVYOPIGA KURA LEO KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA

Image
Wanachama wa Simba wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Klabu ya Simba katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Francis Dande) Wagombea wa nafasi ya Urais katika Klabu ya Simba, Evans Aveva (katikati) na Andrew Tupa na wakipiga kura wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.  Hassan Dalali akipiga kura.  Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu na Rais wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage wakipiga kura.  Rais wa Simba aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage akiagana na mgombea wa Urais wa Simba, Evans Aveva (katikati).  Wagombea wakitafakari.    Wanachama wakihakiki kadi zao. Mgombea wa Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' akizungumza na baadhi ya wanachama kabla ya uchaguzi. Mgombea akiomba kura......Tukiwezeshwa tunaweza.  Mgombea akijinadi.  Mgo...

EVANS EVEVA RAIS WA KWANZA WA SIMBA SC, KABURU NAYE ATISHA..KURA ZA WAJUMBE ZAHESABIWA

Image
  UCHAGUZI mkuu wa klabu ya Simba sc umemalizika salama licha ya changamoto kadhaa kujitokeza na sasa zoezi linaloendelea ni kumalizia kuhesabu kura za wagombea wa nafasi za ujumbe. Kwa nafasi ya Urais, tayari mambo yameshafahamika ingawa taarifa rasmi kutoka kamati ya uchaguzi haijatangazwa. Evans Elieza Aveva ni rais wa kwanza wa klabu ya Simba kwani matokeo ambayo sio rasmi yanaonesha ameibuka na ushindi mkubwa. Aveva amepata kura 1461, huku mpinzani wake pekee, Andrew Peter Tupa akipata kura 381. Wagombea hawa walikuwa na uzito tofauti, kwasababu dalili za Eveva kushinda zilianza siku aliyoenda kuchukua fomu. Hata hivyo ilionekana kungekuwa na mchuano mkali endapo Michael Richard Wambura angeendelea na uchaguzi. Nafasi ya makamu wa rais, aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Simba katika uongozi unaomaliza muda wake, Geofrey Nyange `Kaburu` kwa matokeo yasiyo rasmi ameshinda nafasi hiyo. Matokeo rasmi yatatangazwa muda wowote kutoka sasa, endelea kufuatili...

DIAMOND, MAFIKIZOLO, DAVIDO,TIWA SAVAGE NA FALLY IPUPA KWENYE BET-PRE AWARDS VIP PARTY

Image
Diamond Platinumz anaiwakilisha Tanzania kwenye tuzo za BET zitakazofanyika huko Los Angeles, Marekani .   Jana Diamond akiwa na wasanii wenzake wanaowania tuzo katika kipengele cha International Act (Africa) walihudhuria party ya utangulizi (BET Pre Awards VIP Party). Fally Ipupa aliungana na wasanii wanaowania kipengele kimoja na Diamond ambao ni Davido, Mafikizolo na Tiwa Savage na Sarkodie (hayupo kwenye picha hizi).