MAJINA YA WAJUMBE WATAKAOSHIRIKI KATIKA BUNGE LA KATIBA WATAJWA JIONI HII IKULU DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA UTANGULIZI 1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika. 2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:- (i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; (ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na (iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika. 3. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:- (i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20) (ii)