MIGIRO: NINATAKA KATIBA YA WOTE
Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose Migiro Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa, jana waliapishwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam, kushika rasmi nyadhifa hizo na kuahidi kufanya kazi kwa kasi katika kuwahudumia wananchi. Rais aliwapisha jana jioni Ikulu jijini Dar es Salaam kufuatia mabadiliko aliyoyafanya katika Baraza la Mawaziri juzi na kutangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Dk. Asha Rose Migiro, alisema atahakikisha anajenga misingi kuhakikisha Katiba mpya inakuwa ya watu. Alisema atafanya hivyo, kwa kuwa Katiba siyo ya mtu mmoja wala ya chama kimoja, bali ni ya Watanzania na vyama vyote. Hivyo, alisema atafanya kazi kwa kujituma na kwa umakini mkubwa na kwamba, atazingatia miongozo ya mabadiliko ya katiba kufikia malengo hayo. Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, alisema ameteuliwa na Rais Kikwete kusimamia sera na siyo kuchota fedha katika wizara anayoisi