Posts

MKE ANUNUA TALAKA KWA MILIONI 4

Image
UNAWEZA kusema ni jeuri ya fedha baada ya  mwanamke, Rukia Apach kukubali kulipa shilingi milioni 4 ili apewe talaka na mumewe, Mohamed Kismati baada ya  kuzuiwa kufanya kazi na mkwewe. Ndoa hiyo ilifungwa miaka miwili iliyopita na kufuatiwa na sherehe ya kifahari katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar mwaka juzi. Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao wameachana kwa madai kwamba baba mkwe wa Rukia kukataa mkwewe huyo afanye kazi zaidi ya kuwa mama wa nyumbani. Akizungumza na Ijumaa, Rukia alisema kwamba mumewe alimuahidi kumwendeleza kielimu wakati alipokuwa akisoma kidato cha sita pindi akimuoa. “Awali mume wangu aliniahidi kuniendelea kimasomo, lakini baada ya kuolewa nikakataliwa hata kufanya kazi, amri ambayo ilitolewa na baba mkwe wangu ambaye ni mfanyabiashara,” alisema Rukia. Mwanamke huyo alidai kwamba familia ya mumewe ilishikilia msimamo huo hadi ndoa yao ilipovunjika hivi karibuni. Kama vile haitoshi, Rukia amedai kuwa alilazimika kulipa baadhi ya

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AICHANA CHADEMA TUNDUMA-MOMBA

Image
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana jioni ya leo, amefanya mkutano mkubwa wa hadhara mjini Tunduma, ambao umehudhuriwa na maelfu ya wananchi. Katika mkutano huo uliofabnyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, Kinana aliambatana na majenbe ya Chama cha Mapinduzi , Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro, Katika mkutano huo Kinana amesema wananchi kuikosoa CCM sio kosa kwani Chama hicho kimeingia mkataba na wananchi pale kilipopewa ridhaa ya kuongoza nchi ili kutekeleza ilani yake ya uchaguzi na ni haki ya mtu yeyote wakiwemo wapinzani ili kujua maendeleo yao, Amesema CCM haitakubali kuona ukiritimba na umangimeza wa baadhi ya watendaji Serikalini na unakwamisha maendeleo ya wananchi, ameongeza kuwa kazi ya CCM ni kutenda tu na kazi ya wapinzani ni kusema maneno tu. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadha

RAY NA CHUCHU HANS WAFUMANIWA LIVE

Image
AMA kweli penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Hatimaye uliokuwa uhusiano wa chini kwa chini wa nyota wawili wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans, siyo siri tena baada ya wahusika hao wakuu kujiachia ‘live’, Ijumaa limeshiba. Ray na Chuchu Hans wakiwa katika pozi la kimahaba. KIMAHABA ZAIDI Ishu hiyo ilitokea mapema wiki hii ambapo Chuchu alitundika picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na Ray chumbani kimahaba. Kufuatia tukio hilo kuliibuka gumzo kubwa na kulifanya jambo hilo kuwa ndiyo habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa filamu za Kibongo. Katika picha hiyo, Chuchu anayetumia jina la Chukichuku kwenye Instagram aliambatanisha na maneno yaliyosomeka ‘Me n U’ akimaanisha yeye na Ray hivyo kutoa fursa kwa mashabiki wao kusema chochote. Kwa mujibu wa mashabiki hao, Ray na Chuchu kwa sasa ndiyo love bird au ‘maua’ yanayopendezesha tasnia hiyo. “Mmependezaaa…mapenzi waziwazi,” ilisomeka komenti ya mmoja wa mashabiki hao. “Nilikuwa si

UHURU AHIMIZA KISWAHILI KITUMIWE KUUNGANISHA AFRIKA MASHARIKI

Image
Rais Uhuru Kenyatta akihutubu awali. RAIS Uhuru Kenyatta ametoa wito Kiswahili kitumiwe kuleta umoja baina ya wananchi wa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Akihotubia wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) waliokuwa katika Bunge la Kitaifa Nairobi Jumanne, rais alisema utumizi wa Kiswahili baina ya wananchi wa EAC ni njia mwafaka ya kudumisha utambulisho wa pamoja ulio wa kipekee. “Mungu ametupatia sauti inayoweza kuleta umoja baina ya wananchi wote Afrika Mashariki, na tunafaa tuitumie ipasavyo kupitia vyombo tofauti vya habari ili kutimiza utangamano,” alisema. Hata hivyo, kinaya iliyodhihirika ni kuwa alitoa hotuba yake yote kwa Kiingereza. Rais Kenyatta alitoa hakikisho kuwa juhudi za kutimiza umoja kati ya mataifa ya EAC ziko sambamba, ingawa hakuna usawa kati ya mataifa katika utekelezaji wa mikakati ya kukamilisha juhudi hizo. Alitoa wito kwa wabunge hao w

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA VIJANA WA UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM)

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Beji ya Mapambano dhidi ya Ukimwi na Katibu wa Hamasa na Chipukizi Taifa, Paul Makonda, wakati alipokutana na Vijana hao wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wenye lengo la kusambaza ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Vijana wa UVCCM, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha na OMR makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Vijana wa CCM, baada ya mazungumzo yao alipokutana nao jana kwa ajili ya kumkabidhi ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza

SHIJA ALIZWA NA THEA

Image
Na Gladness Mallya SIKU chache baada ya ndoa ya mwigizaji, Ndubagwe Mithayo ‘Thea’ kuvunjika, mwigizaji Deogratius Shija ‘Shija’ ameibuka na kueleza maumivu anayoyapata juu ya tukio hilo. Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ siku ya ndoa yao. Akizungumza na Amani hivi karibuni, Shija alisema taarifa za kuvunjika kwa ndoa ya Thea na Mike Sangu zilimuuma na kuwataka vijana wengi kuwa makini kabla ya kuoa na haswa kumshirikisha Mungu kila siku kwenye maombi ili ndoa zao zidumu. “Ndoa siyo maigizo. Ndoa ni mkataba mkubwa sana ambao wanaingia wanadamu hivyo inapovunjika huwa haileti picha nzuri kwa Mungu, binafsi inaniuma sana,” alisema Shija.

MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA MTOTO WA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM, PHILP MANGULA, PETER MANGULA, OYSTERBAY DAR JANA

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, wakati alipofika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam,jana jioni kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Peter Mangula, aliyefariki juzi asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili. Peter anatarajia kuzikwa kesho Ijumaa jijini Dar es Salaam.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, marehemu Peter Mangula, wakati alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana jioni kwa jili ya kumpa pole.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phili Mangula, wakati alipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana jioni kwa jili ya kumpa pole.   Maka

BABA KANUMBA AKIMBIWA NA WANAWAKE

Image
Baba wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa. Na Gladness Mallya BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa amefunguka kuwa baada ya kutangaza kuwa wanawake wanaotaka uzao wake wajitokeze azae nao, wamejitokeza kumi lakini akawapa masharti, yakawashinda. Akizungumza na mwandishi wetu, baba Kanumba aliweka bayana kuwa warembo hao waliojitokeza aliwapa sharti la kwenda kupima Ukimwi lakini ajabu wote waliingia mitini. “Wamejitokeza vizuri lakini nashangaa wote wamekuwa wazito katika suala la kupima Ukimwi wameingia mitini, kama wapo wengine watakaolimudu sharti hilo, nawakaribisha,” alisema baba Kanumba.

MTEMVU AFUNGUA NJIA KWA WATANZANIA NAFASI ZA AJIRA UGHAIBUNI

Image
 Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo Job Centre Agency (LTD)Abbas Mtemvu, Akifafanua jambo  Mbele ya waandishi na Wanao Safirishwa na Kampuni hiyo Mwishoni Mwa Wiki Dar es Salaam.    Baadhi ya wahudhuriaji wa tukio hilo  Mmoja wa Wasafiri hao Shamimu Mwarufai  Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD)  Mmoja wa Wasafiri hao Fatuma Chambo  Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD)   Dominica Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD) kwa niaba ya Tabu Khalfani  Lita  Dominik Akikabidhiwa Tiketi na Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agncy (LTD) kwa niaba ya Tabu Khalfani mwishoni mwa wiki Dar es Salaam.  Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Bravo Job Centre Agnc

ONA MAUNO KATIKA WIMBO WA SNURA "NIMEVURUGWA"

NORA AWANANGA RAY NA JOHARI

Image
Musa Mateja na Gladness Mallya BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ kueleza mazito kuhusu Ray, Johari na Chuchu Hans, msanii mwenzake, Nuru Nassoro ‘Nora’ naye amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya nyuma itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao. Nuru Nassoro ‘Nora’. Akizungumza na mapaparazi wetu hivi karibuni, Nora alisema Ray na Johari walimfanyia ‘mambo mabaya’ yaliyosababisha kupotea kabisa kwenye sanaa ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni. Johari. “Kinachowasumbua Ray na Johari ni laana yangu na kweli nimeamini Mungu analipa hapahapa duniani kwani walinifanyia mambo ya ajabu, wakanipoteza kabisa kwenye fani, walinifanya nichanganyikiwe wakijua sitapona, lakini sasa hawaelewani tena wakati walikuwa wanapendana kama pete na kidole. “Nakumbuka zamani nilikuwa nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye akamnunulia Johari kama hizo za kwangu, alimtengeneza Johari akawa anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndiyo mimi

Wema Sepetu ajuta kutumia mikorogo, aanza kuitamani ngozi yake ya awali

Image
Wema Sepetu ambaye ni Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu anajuta kutumia mkorogo na hatimaye kupoteza urembo wake wa asili aliokuwa nao mwanzo kabla ya kuanza kujichubua.    Chanzo kimoja makini ambacho kipo karibu na Wema na ambacho pia ni star wa filamu kimetutonya kuwa Wema anajuta kujichubua na hajiamini tena katika urembo tofauti na miaka ya nyuma kwani kila mtu sasa hivi anajua Wema ni fake na amejaa urembo wa kichina kwa aslimia kubwa.

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA MAOMBOLEZO KUFAUTIA MSIBA WA MZOBORA

Image
Marehemu  Dunia Mzobora enzi za uhai wake. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kufuatia kifo cha Mwandishi wa Habari na Msanifu wa Habari Msaidizi Mkuu wa Gazeti la Uhuru, Bwana Dunia Mzobora, kilichotokea tarehe 27 Novemba, 2013 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya shinikizo la damu. Marehemu aliajiriwa katika Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mwaka 1989 kama Mwandishi wa Habari Mwanafunzi, kisha akaendelea kupanda ngazi hadi kufikia cheo cha Msanifu wa Habari na hatimaye kuwa Msanifu Mkuu Msaidizi, cheo alichokuwa akikishikilia hadi mauti yalipomkuta. “Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha mmoja wa Waandishi wa Habari Shupavu na Mchapakazi, Dunia Mzobora aliyekuwa akilitumikia Gazeti la Chama Cha Mapinduzi (CCM) la UHURU, kilichosa

SIRI 5 ZA WOLPER ZAVUJA .... HIZI HAPA ALIVYOZIANIKA

Image
MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili. Wolper akifunguka ndani ya Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar. Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni,… Na Sifael Paul MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili. Wolper akifunguka ndani ya Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar. Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwen