Posts

SAFISHA MACHO MTU WANGU WA NGUVU

Image
baada ya uchovu wa foleni sina budi kupunga upepo kwa muda

LADY JAY DEE AMVAA JANUARY MAKAMBA LIVE

Image
Lady Jaydee Lady Jaydee kweli ni Anaconda na sio mtu wa kuchezea kwani ukiingia kichwa kichwa kwenye kumi na nane zake anakumeza na kukupaka live kama huna hoja ya msingi. Hayo yamempata Mbunge wa Bumbuli January Makamba. Angalia alichoandika Makamba hapo chini na jibu la Lady Jaydee ambaye ni mwanamuziki mwenye jina kubwa Afrika mashariki.

MSANII SNURA AFIWA NA KAKA YAKE WA TUMBO MOJA APATWA NA AJALI YA RADI MLANDIZI

Image
 msanii SNURA kafiwa na kaka yake wakuzaliwa nae anaejulikana kwa jina la Yusufu kaka yake wa kwanza kuzaliwa kwa marehemu baba yake mzee Mushi. Msiba huo umetokea Mlandizi baada ya kupigwa na radi kali jana asubuhi wakati marehemu akiwa shambani kwake Mlandizi. SNURA akiongea na blog hii  amesema wanazika leo huko huko Mlandizi mida ya saa kumi jioni.   Mungu alaze roho ya maehemu YUSUFU MUSHI mahala pema peponi. AMIN

MTOTO MIAKA 6 ALAWITIWA, AHARIBIWA!

Image
Stori: Joseph Ngilisho, Arusha   Dunia haina huruma! Mtoto wa kiume ambaye ni denti wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka sita anayesoma katika shule moja ya msingi iliyopo Olasiti jijini hapa, anadaiwa kulawitiwa hadi kuharibiwa vibaya sehemu za siri. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililotokea hivi karibuni, inadaiwa kuwa kitendo hicho kilifanywa na kinyozi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50. Akizungumza akiwa na shangazi yake  katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru alikolazwa akipatiwa matibabu, mtoto huyo alimtaja mtuhumiwa kwa jina moja la Abuu, mkazi wa eneo hilo ambaye alimrubuni mwathirika huyo kwa ofa ya kumnyoa nywele. Alidai Abuu amekuwa akimfanyia mchezo huo mchafu majira ya mchana au usiku katika nyumba ambayo haijamalizika kujengwa (pagale) na wakati mwingine humzungusha nyuma ya saluni yake. Ilidaiwa kuwa hali ilikuwa mbaya baada ya mtoto huyo kushindwa kutembea na kutokwa na haja kubwa bila mpangilio

Malkia wa nyuki aandika barua kujitoa Simba

Image
Malkia wa Nyuki akiwa ofsini kwake. Na Mwandishi Wetu MALKIA wa Nyuki ameandika barua ya kujiondoa kwenye Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba kutokana na kuchukizwa na migogoro. Malkia ambaye jina lake halisi ni Rahma Al Kharusi, amethibitisha hilo na kusema aliamua kufanya hivyo kutokana na kukerwa na migogoro ndani ya kamati hiyo. Akizungumza jana kutoka Oman, Malkia wa Nyuki alisema aliamua kujiondoa kwa mambo mawili makubwa ambayo ni migogoro na kukosa nafasi. “Baada ya kumueleza Rage kwamba nimefikia uamuzi huo, ameniomba nibaki kwa kuwa ninahitajika Simba. Kanishauri kwamba niingie katika upande wa baraza la wadhamini. Kwangu naona si mbaya, maana sitakuwa na vikao vya mara kwa mara, lakini bado nasisitiza migogoro si sahihi,” alisema.   “Kwani kama si kuteuliwa katika nafasi hii ya kusimamia mali za Simba, basi nilikuwa nimeshajiondoa kabisa Simba hadi hapo hali itulie maana

MH. LOWASSA AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA KATA YA SARANGA,KIMARA JIJINI DAR

Image
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiburudika kwa kucheza muziki sambamba na wakina Mama wakazi wa Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam,Mwishoni mwa wiki wakati alipokwenda kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo.Zaidi ya Sh. Mil. 100 ziliweza kupatikana kwenye harambee hiyo.  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipena mikono na Wakazi mbali mbali wa Kata ya Saranga,Kimara wakati akiendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki.  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisisitija jambo kwa wananchi wakazi wa Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya p

KINANA AANZA ZIARA RASMI MKOANI MBEYA

Image
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ipinda wilayani Kyela kwenye mkutano wa hadhara ambao ndio mkutano wake wa kwanza kama Katibu Mkuu wa CCM lakini pia ndio siku aliyowasili akitokea Ruvuma .  Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakazi wa Ipinda wilaya ya Mbeya na kuwasihi wakina mama wawe mstari wa mbele kuhakikisha mabinti zao wanapata elimu.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Ipinda na kuwaeleza mambo muhimu ya kutafakari kabla hawjakurukupia siasa na baadhi ya vyama vingi vipo kwenye mfumo na utawala binafsi.  Mbunge wa Kyela Dk. Harisson Mwakyembe akihutubia wakazi Ipinda wa kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa Nyumbani kwa Balozi wa Nyumba 10 Ndug

IZZO B AKUMBWA NA BALAA LA KUKOMBWA KILA KITU ... ISHU NZIMA HII HAPA

Image
Rapper Izzo Bizness asubuhi ya leo ametoa taarifa kuwa internet cafe yake iliyopo Mbeya eneo la chuo cha TEKU imevunjwa na wezi na computer sita zimeibiwa. Ameomba raia wa Mbeya kutoa taarifa wanaposikia mtu anauza computer pasipo njia halali. Soma Hapa Alichoandika Izzo B. #PoleBro

tff yaunda KAMATI NDONGONDOGO

Image
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametangaza wajumbe wa kamati ndogongo (standing committees) wakati zile za haki (judicial organs) na uchaguzi zitaundwa baadaye. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika leo (Novemba 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Rais Malinzi alisema kamati hizo zimeundwa kwa mujibu wa katiba ili kuisaidia Kamati ya Utendaji. Pia ametangaza wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji aliowateua. Wajumbe hao ni Richard Sinamtwa na Ramadhan Nassib, wakati wengine wanaoingia moja kwa moja kwenye Kamati ya Utendaji kutokana na kamati wanazoziongoza ni Dk. Paul Marealle na Saloum Umande Chama. Kamati ya Fedha na Mipango inaongozwa na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava. Geofrey Nyange anaongoza Kam

BREAKING NEWS: GARI LILILOBEBA MABOMBA YA GESI LAPATA AJALI NA KUPINDUKA HUKU MTU MMOJA AKIRIPOTIWA KUFARIKI DUNI

Image
  Mmoja ya malori yanayofanya kazi ya kusimba mabomba ya gesi kati ya Lindi na Mtwara imepata ajali katika kijiji cha Mnolewa na mtu mmoja ameripotiwa kufariki dunia. chanzo lindiyetu.  

ZITTO KABWE: SIONDOKI CHADEMA NG'O

Image
Zitto Kabwe akielezea kwa wanahabari kuwa haondoki Chadema kamwe. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema haondoki Chadema ng'o. Adai yeye ni mwanachama halali wa chama hicho, amejiunga na Chadema akiwa na umri wa miaka 16, maisha yake yote ameyatoa kwa ajili ya kukitumikia chama hivyo hawezi kuondoka Chadema. Ameyasema hayo muda huu wakati akiongea na wanahabari katika chumba cha mkutano kilichopo katika Hoteli ya Serena Posta jijini Dar es Salaam. Dk. Kitila Mkumbo akiwaeleza wanahabari kuwa Zitto Kabwe hausiki na 'Waraka wa Siri'. Naye Dk. Kitila Mkumbo aliyevuliwa ujumbe wa Kamati Kuu Chadema amekubali kuwa 'Waraka wa Siri' uliosomwa kwa wanahabari na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu juzi na kusababisha kuwavua vyeo Zitto Kabwe, yeye na Samson Mwigamba ni yeye aliyeuandaa lakini Zitto Kabwe hausiki

WAREMBO WALIVYOPAGAWA KWA P-SQUARE, MMOJA APACHIKWA JINA LA 'ONYINYE' NA KUZAWADIWA SAA YA BEI MBAYA!

Image
Mrembo aliyechunukiwa na Peter akiwa jukwaani baada ya kuitwa na kujitokeza ....akinyoosha mkono… Mrembo aliyechunukiwa na Peter akiwa jukwaani baada ya kuitwa na kujitokeza ....akinyoosha mkono ...akivishwa saa ya bei mbaya na Peter, ambaye alisema ameoa Nigeria wiki iliyopita na Bongo anaoa pia..... ....sogea nikubusu my 'Beautiful Onyinye....! ....mmmwaaaa!!! ....ni kama anamnong’oneza ‘jamani Peter wewe si unanitafutia balaa na mkeo’....hahahahaha!!! ....this is my beautiful Onyinye oooo!!  ".....oooo 'tank' you 'tank' you my Onyinye......!!" .....Mr. P is getting back to business now, lol!!  .....akiimba kwa hisia kali! ...o!o!o!o!, this guy yooo, is crying oohhh!!!  .......jukwaa lilikuwa lao, walilitawala walivyotaka!  ...hapa kazi ni kazi tu!