Malkia wa nyuki aandika barua kujitoa Simba

Malkia wa Nyuki akiwa ofsini kwake.

Na Mwandishi Wetu
MALKIA wa Nyuki ameandika barua ya kujiondoa kwenye Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba kutokana na kuchukizwa na migogoro.
Malkia ambaye jina lake halisi ni Rahma Al Kharusi, amethibitisha hilo na kusema aliamua kufanya hivyo kutokana na kukerwa na migogoro ndani ya kamati hiyo.
Akizungumza jana kutoka Oman, Malkia wa Nyuki alisema aliamua kujiondoa kwa mambo mawili makubwa ambayo ni migogoro na kukosa nafasi.
“Baada ya kumueleza Rage kwamba nimefikia uamuzi huo, ameniomba nibaki kwa kuwa ninahitajika Simba. Kanishauri kwamba niingie katika upande wa baraza la wadhamini. Kwangu naona si mbaya, maana sitakuwa na vikao vya mara kwa mara, lakini bado nasisitiza migogoro si sahihi,” alisema.

 
“Kwani kama si kuteuliwa katika nafasi hii ya kusimamia mali za Simba, basi nilikuwa nimeshajiondoa kabisa Simba hadi hapo hali itulie maana sioni faida ya haya yaliyopo sasa.”
Malkia wa Nyuki, ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Simba, ndiye alitoa zaidi ya Sh milioni 80, Simba ikaweka kambi ya siku 15 jijini Muscat nchini Oman.
Lakini aliahidi kuanza kushughulikia kujenga uwanja kwa ajili ya mazoezi, pia alifunga safari kwenda kufanya mazungumzo na Sunderland kuisaidia Simba, lakini amekuwa akilalama kwamba migogoro na utendaji mbovu ni tatizo.
Katika mkutano wa jana jijini Dar, Rage alitangaza kumteua Malkia katika nafasi hiyo na nafasi yake katika kamati ya utendaji akamteua Michael Richard Wambura aliyewahi kuwa katibu mkuu Simba.CHANZO GPL

Comments

Popular posts from this blog