Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay akabidhiwa Barcode yake
Mwanamuziki Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi yenye Barcode ambazo amekabidhiwa leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili kuchukua Barcode za Tanzania katika sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini. Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye Koti la suti) akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi toka GS1 Tanzania na kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka Profesa Jay. Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano wa hundi yenye Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Pfofesa Jay huku wajumbe wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia. Wanamuziki nchini wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo kwa kujitangaza na kutanua wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya Barcode.