MCHUNGAJI ATOA SIRI ALIVYOJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA
Mchungaji Donald Mwakisambwe wa kanisa la Kipendekoste la Kiinjili Tanzania, kwenye ofisi za gazeti hili wakati akitoa ushuhuda wa kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya. Kinara wa kimataifa wa kuuza madawa ya kulevya aliyezunguka sehemu mbalimbali duniani kuuza mihadarati, ameacha biashara hiyo na sasa anahubiri Injili kupiga vita dawa hizo. Kigogo huyo Mtanzania na mzaliwa wa Mbeya, ambaye sasa anajiita kiumbe kipya katika Kristo, ni Mchungaji Macdonald Mwakisambwe wa Kanisa la Kipentekoste la Kiinjili jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika mahojiano maalumu Jumamosi jana, Mwakisambwe alisema alianza biashara ya unga mwaka 1990 na kuifanya kwa miaka 10, akisafirisha dawa kwa maelfu ya wateja walioko Afrika, Asia, Ulaya na Amerika. Alisema katika kutimiza azma hiyo, alitumia pasi za kusafiria za mataifa mbalimbali zenye majina tofauti, zikimuonyesha kuwa ni raia wa Msumbiji, Tanzania, Kenya, Namibia, Afrika Kusini na Namib