JAJI BOMANI AVIONYA VYOMBO VYA USALAMA

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1638570/highRes/434731/-/guqhon/-/jaji_bomani.jpg
Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji Mark Bomani, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo kufuata misingi ya sheria katika utendaji wao wa kazi. Jaji Bomani amevitaka pia vyombo vya usalama vya Tanzania kuzingatia sheria katika matumizi ya silaha kwenye matukio mbalimbali wanayokabiliana nayo. Kauli hiyo ameitoa wakati wa Kongamano la Maadili ya Waandishi wa Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam likiwa na kaulimbiu ya 'Wajibu wa Vyombo vya Habari Kupambana na Kauli za Chuki na Itikadi Kali.' Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Tanzania ameongeza kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya vyombo vya dola kuwapiga watu bila kufuata sheria ambazo zinakataza kufanya hivyo, lakini mambo hayo yanatokana na uelewa mdogo. Amesema,  hata maandamano na mikutano yoyote inapozuiwa pia ni lazima vigezo na sheria zifuatwe ili kila mmoja au kinachofanyika kimezingatia sheria na si uonevu au upendeleo.

Comments

Popular posts from this blog