Posts

JAJI BOMANI AVIONYA VYOMBO VYA USALAMA

Image
Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji Mark Bomani, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo kufuata misingi ya sheria katika utendaji wao wa kazi.  Jaji Bomani amevitaka pia vyombo vya usalama vya Tanzania kuzingatia sheria katika matumizi ya silaha kwenye matukio mbalimbali wanayokabiliana nayo. Kauli hiyo ameitoa wakati wa Kongamano la Maadili ya Waandishi wa Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam likiwa na kaulimbiu ya 'Wajibu wa Vyombo vya Habari Kupambana na Kauli za Chuki na Itikadi Kali.' Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Tanzania ameongeza kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya vyombo vya dola kuwapiga watu bila kufuata sheria ambazo zinakataza kufanya hivyo, lakini mambo hayo yanatokana na uelewa mdogo. Amesema,  hata maandamano na mikutano yoyote inapozuiwa pia ni lazima vigezo na sheria zifuatwe ili kila mmoja au kinachofanyika kimezingatia sheria na si uonevu au upendeleo.

soma vichwa vya magazeti leo jumapili 1/9/2013

Image

RWANDA YAPELEKA WANAJESHI 1700 KUWASAIDIA WAASI WA M23 BAADA YA KUELEMEWA NA JWTZ ( MONUSCO)

Image
KIKUNDI cha waasi cha M23 kinachopambana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kimeripotiwa kupigwa vibaya na kutikisa nguvu za kikundi hicho kutokana na baadhi ya wapiganaji wake kuripotiwa kupoteza maisha.   Mapigano baina ya M23 na Jeshi la Serikali ya DRC linalosaidiwa na Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO), yameibuka upya ndani ya wiki hii.   Habari za kiintelijensia  zinasema kuwa, kutokana na shambulio hilo, Serikali ya Rwanda imelazimika kuingilia kati kusaidia waasi hao kwa kupeleka bataliani mbili zenye jumla ya askari 1,700 huko DRC , ili waweze kukabiliana na nguvu ya majeshi ya JWTZ, DRC, Monusco na Brigedi ya Majeshi ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa yenye mamlaka ya kujibu mapigo (FIB). Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, Rwanda imepeleka bataliani hizo mbili zenye askari 850 kila moja saa 48 zilizopita na kwamba wamevuka mpaka kuingia DRC katika eneo la Kibumba, lakini wanashindwa...

Mechi za Leo ligi kuu Uingereza...!

Image
15:30 Liverpool vs Manchester United (P.T) 15:30 West Bromwich Albion vs Swansea City

MWANAMKE ABAKWA NA KUCHOMEKWA KISU SEHEMU ZA SIRI.

Image
Ukatili dhidi ya wanawake  umeendelea  kushika  kasi  ya  ajabu katika  bara  la  Afrika..... Ukatili  huo  unajidhirisha  baada ya  ongezeko  kubwa  la  matukio  ya  ubakaji  yanayoambatana  na  mauaji  ya  kikatili  kama  njia  mojawapo  ya  kuficha  ushahidi. Wiki  hii  mitandao  ya  nchini  Ghana  imeripoti  juu  la  tukio  la  mwanamke  mmoja  aliyebakwa  na  kuuawa  kikatili  kwa  kuchomwa  kisu  tumboni  na  sehemu  za  siri... <<  PICHA  YA   MWANAMKE  HUYO>> Picha  ya  tukio  hilo  ni mbaya. BOFYA  HAPO  JUU  KUIONA  PICHA...

MANSOUR AKATAA KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA UAMUZI WA KUFUKUZWA CCM

Image
Aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilisihi Jimbo la Kiembe Samaki (CCM) Mansour Yussuf Himid amesema licha ya kufukuzwa Uanachama katika chama hicho hatoenda Mahakamani kutetea nafasi hiyo kwani kufanya hivyo ni kukaribisha Malumbano ambayo hayana tija. Amesema kwenda kupinga uamuzi huo Mahakamani ni kuhalalisha yeye kuwa Mwakilishi wa Mahakama badala ya Wananchi jambo ambalo hapendelei kutokea katika maisha yake. Mansour ameyasema hayo leo katika Kongamano la Kamati ya Maridhiano lililofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. Amesema amekuwa akiulizwa Maswali mengi na Watu tofauti kuhusu mustakabali wake kisiasa baada ya kufukuzwa uanachama na kuongeza kuwa hana Pesa za kuchezea kwenda kupinga uamuzi wa Chama cha Mapinduzi Mahakamani. "Wenzangu wamenipima na wameniona sifai ni haki yao, siendi Mahakamani, sina pesa za kuchezea wala sitaki kuwa Mwakilishi wa Mahakama" Alisema Mansour. Mansour aliyejiung...

Maandalizi ya Kili Music Tour Kigoma yanavyoendelea

Image
 Kazi ya kufunga jukwaa na banner za kikwetu kwetu

SHULE YAWAZUIA ROBO TATU YA WANANFUNZI KUFANYA MITIHANI.

Image
Katika hali isiyokuwa ya kawaida robo tatu ya wanafunzi katika shule ya sekondari Uhuru, Manispaa ya Shinyanga wamezuiwa kufanya mitihani ya muhula wa pili kwa madai ya wazazi wao kushindwa kulipia michango Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waliozungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa walisema pamoja na kuzuiwa kufanya mitihani hiyo walimu wao waliwapa adhabu ya kukaa chini wakiwa juani na baadae walipewa kazi ya kumwagilia bustani wakati wenzao wachache wakiendelea na mitihani. Mmoja wa wanafunzi hao (jina tunalo) alisema walielezwa na walimu wao kwamba ye yote ambaye hatokuwa amelipa ada na michango mbalimbali shuleni hapo ikiwemo mchango wa mlinzi hatoruhusiwa kufanya mitihani hiyo mpaka pale wazazi wao watakapokuwa wamelipa michango wanayodaiwa. Mwanafunzi huyo alifafanua kuwa hata pale walipojaribu kuwaomba walimu wawaruhusu kufanya mitihani kwa vile suala la michango si jukumu lao bali la wazazi wal...

WADAU WA UTOAJI HAKI WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE NCHINI WAKUTANA KUJADILI UTOKOMEZAJI WA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA YANAYOAMBATANA NA RUSHWA YA NGONO

Image
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA),mama Salma Kikwete (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono mara baada ya kukabidhiwa kitabu cha mwongozo wa namna ya kushughulikia mashauri mbalimbali ya kisheria alichokabidhiwa na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania Mh. Jaji Engera Kileo  leo jijini Dar es salaam. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete akifungua warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo jijini Dar es salaam. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Bi. Salome Anyoti Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masual...

AJINYONGA NJE YA UKUMBI WA DISKO, MAMA AKATAA

Image
KULWA Shaban (18) mkazi wa Gongo la Mboto, jijini Dar amedaiwa kujinyonga na mwili wake kukutwa  ukinin’ginia kwenye mti pembezoni mwa ukumbi wa disko maarufu kwa jina la Majita. Akizungumza kwa machungu, mama wa kijana huyo, Rehema Omar alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo siku nne kabla ya kukutwa akiwa amejinyonga, Kulwa aligombana na baadhi ya marafiki zake ambao walichukua tofali na kumpiga nalo mdomoni na kusababisha meno mawili  kung’oka. “Tulimpa fedha kwa ajili ya kwenda kujitibia kisha alirejea nyumbani na kuendelea kujiuguza majeraha kwani yalikuwa ni makubwa,” alisema Rehema.NA GLOBAL PUBLISHER Mama huyo aliendelea kusema wakati mwanaye akiendelea kuuguza kidonda ndipo alipopatwa na maswahibu hayo baada ya kwenda disko na wenzake. “Siku hiyo niliingia kulala na ilipofika saa tisa usiku niligongewa mlango na watu wawili na kuambiwa hali ya mtoto wangu ni mbaya  pasipo kubainisha amefanya nini,” ...

PICHA YA MWANAUME ALIYEGEUZWA KUWA MWANAMKE BAADA YA KUZINI NA MKE WA MTU

Image
Mwanaume  mmoja  nchini  Kenya  amejikuta  akiambulia aibu  ya  mwaka  baada  ya  uume  wake  kubadilishwa  kuwa  uke.... Mwanaume  huyo  anadaiwa  kufanyiwa  mchezo  huo  baada  ya  kufumaniwa  akizini  na  mke  wa  mtu  katika  kitanda  cha  mumewe... Taarifa  zinadai  kwamba, mume  huyo  alipomfumania  mkewe  hakufanya  vurugu  yoyote  na  badala  yake  alitoweka  na  kwenda  kwa  mganga  wa  jadi  ambaye  aliuchukua  uke  wa  mkewe  na  kuupachika  katika  uume  wa  mzinzi  huyo. Picha  ni  ya  aibu  sana.BOFYA  HAPO  CHINI <<  BOFYA  HAPA  KUONA  PICHA>>

AIBU....AIBU.....AIBU........NANDO AKAMATWA BAADA YA KUIBA CAMERA MOJA YA BIG BROTHER....

Image
Nando  ameendelea  kuitia  aibu  Tanzania  baada  ya  kukumbwa  na  kashfa  mpya  ya  wizi  wa  kamera  ndani  ya  jumba  la  big  brother. Wizi  huo  unadaiwa  kutendeka  baada  ya  Nando  kualikwa  kushiriki  fainali  za  Big brother  ambapo Dillish aliibuka  mshindi  wa  shindano  hilo..... Baada  ya   wizi  huo, kamera  za  jumba  hilo  zilimuumbua.Nando  alikamatwa  na  kuamriwa  airejeshe  camera  hiyo. Source:  << BIG BROTHER>>

TAZAMA JINSI WEMA SEPETU ALIVYOMTOA MACHOZI MAMA KANUMBA...!!

Image
 Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu akimtunza mama yake Kanumba Flora Mtegoa a.k.a. Mama mkwe wake mara baada ya mama huyu kumfwata msanii huyo wakati alipokuwa akicheza muziki uliokuwa ukitumbuizwa na Machozi Bendi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa filamu ya Foolish Age iliyoandaliwa na msanii mwenzao Elizabety Michael 'Lulu'  Wema Sepetu akimfuta machozi mama yake Kanumba, Flora alijikuta akishindwa kuzuia hisia zake baada ya kutunza kiasi cha fedha cha kutosha kabisa kwa matumizi hata ya wiki nzima na mwanadada huyo Wema akionyesha heshima kwa kumpigia magoti mwanamama huyo ambaye alishawahi kuwa mkwe wake kipindi hicho

Wakali Wa Kili Music Tour Watembelea Makumbusho ya Doctor Livingstone Kigoma

Image
Kundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajili ya onyesho hilo. Wasanii hao  8 ni kati ya 12 watakaopanda katika jukwaa moja uwanja wa Lake Tanganyika siku ya Jumamosi. Kundi la pili la wasanii ambao ni Profesa Jay, Diamond, Lady Jaydee na Barnaba wanatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi asubuhi. Baada ya kupata mlo wa mchana ulioandaliwa na mwenyeji wao ambaye ni  Doctor Gerrard Mipango wasanii hao walipata nafasi ya kutembelea makumbusho ya Doctor Livingistone yaliyoko Ujiji na kujionea historia mbalimbali ya mzungu huyo anayetambuliwa kama mvumbuzi wa Ziwa Tanganyika na pia kuona maeneo biashara ya utumwa ilipokuwa ikifanyika na kujifunza kuhusu asili ya wenyeji wa Mkoa wa Kigoma.