Posts

Mchakato wa kumrejesha Alex Massawe waiva

Image
Mchakato wa kumrejesha nchini, mfanyabiashara maarufu Alex Massawe, aliyekamatwa Dubai, Falme za Kiarabu, umeanza rasmi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutoa hati ya kumkamata na kumrejesha nchini kujibu mashtaka. Hati hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Geni Dudu, kufuatia maombi ya Jamhuri, yaliyotolewa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka, baada ya kumfungulia kesi ya jinai. Katika kesi hiyo namba 150 ya mwaka 2013, Massawe anakabiliwa na mashtaka ya kughushi na kuwasilisha hati za nyumba. Massawe ambaye alikamatwa hivi karibu na Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol), amekuwa akitafutwa akihusishwa na matukio ya uhalifu. Mahakama hiyo ilitoa usahihi wa majina yake, kuwa ni Alex Siryamala Massawe. Kwa mujibu wa Kweka, mtuhumiwa anayeshikiliwa katika nchi nyingine anapoombwa kurejeshwa nchini,lazima kuwe na kesi ambayo anatakiwa kujibu mashtaka, vinginevyo inaweza kuwa vig

Ndege ya Rais yadaiwa kubebea mkaa

Image
Wabunge wa CCM Zanzibar wameibua zengwe jipya dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad kwamba anatumia ndege ya Rais kubebea mkaa, mihogo na ndizi kutoka Pemba kwenda Unguja. Habari zilizopatikana kutoka ndani ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinaeleza kuwa, tuhuma hizo zilitolewa na wabunge hao wakati wa kikao chao na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein mwezi uliopita. Kitendo hicho kinachodaiwa kufanyika mwezi uliopita kimeonekena kuwakera baadhi ya viongozi wa Serikali wakiwamo wabunge wa CCM Zanzibar, ambao wakati wa kikao hicho na Rais Dk Shein mwezi uliopita mjini Zanzibar, walilizungumza kwa uchungu na kuomba Rais amuonye Maalim Seif kwa kuigeuza ndege ya Rais kuwa ya mizigo. Anayedaiwa kuibua hoja hiyo ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Khamis, ambaye alisema kuwa kitendo hic

Washauri wa rais Obama wakutana kuijadili Syria ;

Image
Washauri wa rais Barack Obama watakutana katika ikulu ya Marekani ya White House mwishoni mwa wiki hii kujadili nafasi mbali mbali za nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na hatua za kijeshi, dhidi ya serikali ya Syria. Washauri wa rais Barack Obama watakutana katika ikulu ya Marekani ya White House mwishoni mwa wiki hii kujadili nafasi mbali mbali za nchi hiyo , ikiwa ni pamoja na hatua za kijeshi , dhidi ya serikali ya Syria. Mjadala huo utahusu iwapo serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali katika shambulio mapema wiki hii. Maafisa wa Marekani wamesema jana Ijumaa(23.08.2013) kwamba iwapo rais Obama atashiriki katika mkutano huo , hali inayoonekana kuwa kuna uwezekano , itakuwa kikao chake cha kwanza kamili akiwa na wasaidizi wake wa ngazi ya juu wa sera za mambo ya kigeni tangu shambulio la gesi ya sumu siku ya Jumatano katika kitongoji kimoja mjini Damascus. Uamuzi bado Lakini afisa huyo ambaye amezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, ametahadharisha dhidi ya

Mapigano yazuka tena Kongo

Image
Mapigano yanayoendelea baina ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika eneo la Kibati karibu na mji wa Goma, yanatajwa kuwa yamewaathiri raia katika eneo la mapigano. Mji wa Goma ulipigwa na mshituko jioni jana, pâle mabomu yalipokuwa yanavurumishwa katika mji huo. Ni kata za Katindo ya kushoto pamoja na Murara ndizo ziliathirika na mabomu hayo. Katika kata la Murara, duru toka machifu wa kata hizo zadokeza, kuwa watu watano ndio walijeruhiwa mukiwemo watoto watatu ambao hali yao ni m

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image

SERENGETI FIESTA 2013 TABORA NOMAA SANAAA YAWASHA MOTO USIKU KTK UWANJA WA AL-HASSAN MWINYI

Image
Abdul Kiba,msanii wa muziki wa bongofleva akiimba mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.  Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.  Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia mbele ya wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Pr

FOOLISH AGE YA LULU MICHAEL YAPIGWA STOP KUTOKANA NA MAVAZI YA NUSU UCHI YALIYOTUMIKA.

Image
Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana na taratibu zote alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu yake ya “Foolish Age”. Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe pamoja na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo muhimu ya kufanyiwa marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya “Foolish Age” katika Bodi ya Filamu kwa ajili ya ukaguzi. Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni ya Proin Promotions ikiwasilisha filamu yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi. Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza nchini imeipiga stop filamu ya Foolish age ya msanii wa kike mwenye mvuto Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kukuta picha zilizo nje ya maadili ya Kitanzania katika filamu hiyo.... Filamu hiyo ambayo ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe

MCL sasa kuwajaza wasomaji mamilioni, magari matatu;

Image
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), imezindua promosheni kabambe ya 'Chomoka na Mwananchi' itakayowawezesha wasomaji wa gazeti la Mwananchi, kujishindia zawadi zenye thamani ya Sh250,000,000.Zawadi hizo ni pamoja na fedha taslimu na magari matatu mapya. Akizungumza katika uzinduzi huo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Tido Mhando, alisema promosheni hiyo itakayoanza leo, itafanyika nchini kote kwa siku 100 na kila siku kutakuwa na mshindi ambaye atajinyakulia Sh1,000,000. P.T "Hii ni promosheni ambayo lengo lake ni kuwashukuru wasomaji wetu kwa kuendelea kulipenda gazeti lao na kuliweka juu hapa nchini," alisema Mhando. Alisema hadi mwisho wa promosheni hiyo (Novemba 30, mwaka huu), wasomaji 100 watakuwa wamejinyakulia fedha taslimu Sh100,000,000 na wengine watatu watapata magari mapya. "Lengo letu ni kuwawezesha wasomaji siyo tu kupata habari na kufikiri tofauti, bali pia kuweza kuwajenga kimaisha," ali

Miss Tanzania 2012 aanza ujenzi wa bweni la Albino Shinyanga

Image
Brigette Alfred pamoja na baadhi ya wanafunzi walemavu wa ngozi wa shule ya msingi Buhangija wakinyanyua moja kati ya mabati 200 aliyonunua kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana katika shule hiyo,CHANZO:Majuto Omary. Na Mwandishi wetu, Shinyanga MREMBO wa Tanzania, Brigitte Alfred ameonyesha mfano wa kuigwa nchini katika tasnia hiyo baada ya kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (albino) katika wilaya ya Shinyanga wanaoishi katika shule maalum ya Buhangija. Tayari mrembo ameweka jiwe la msingi na kupandisha ukuta sambamba na kukabidhi mabati 200 kwa ajili ya kujengea paa la bweni hilo la wavulana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 50. Makabidhiano hayo yalifanywa na mrembo huyo kwa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi, afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na mwalimu mkuu, Peter Ajali. Briggite alisema kuwa ameamua ku

CLOUDS MEDIA GROUP YAANDAA SEMINA YA FURSA MKOANI TABORA LEO

Image
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Diamond, akiwaimbisha washiriki wa semina ya Fursa waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye ukumbi wa Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora, kushoto kwake ni Bwa. Marco Vingila kutoka shirika la TPSF. Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa msisitizo, masuala ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika suala zima la ujasiliamali mapema leo kwenye semina ya Fursa iliyofanyika katika ukumbi wa Student's Center, uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group, imefadhiriwa na shirika la NSSF; Zantel, MaxMalipo, Lake Oil.  Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakishiriki semina ya Fursa kwa vijana ililiyofanyika leo kwenye ukumbi wa Student's Center katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo, kutoka kulia ni Msanii Godzilla, Baba Levo, Amin

EDWARD LOWASSA AMBANA BERNAD MEMBE KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE

Image
 Mhe. Edward Lowassa (Mb.)Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  na Mbunge wa Monduli akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kupitia Taarifa ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ya Wizara. Kikao hicho kilifanyika katika  Ofisi Ndogo za Bunge tarehe 19 Agosti, 2013.   Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwasilisha  Taarifa ya Wizara ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge (hawapo pichani).   Baadhi ya Waheshimiwa wa Wabunge ambao pia  ni Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).  Kikao kikiendelea. Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa karibu taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe