Posts

ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA

Image
Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita. Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika  kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam. Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu. Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi. BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.  MJUE ASKOFU MOSES KULOLA Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya mi

SHEIK PONDA AFIKISHWA MAHAKAMANI TENA.....KESI YAAAHIRISHWA HADI SEPTEMBA 11

Image
Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda jana alisababisha kusimama kwa shughuli za Serikali wilayani Morogoro baada ya ofisi kadhaa ikiwamo ya Mkuu wa Wilaya na baadhi ya mitaa kufungwa ili kupisha kusikilizwa kwa kesi inayomkabili katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro.    Tofauti na Agosti 19, mwaka huu wakati aliposafirishwa kwa helikopta, jana Sheikh Ponda alisafirishwa kwa barabara kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro akiwa chini ya ulinzi. Mbali ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro kufungwa, nyingine ni Hazina Ndogo, Madini, Posta, Vipimo, Ukaguzi na Maktaba ya Mkoa.   Sababu za kufungwa kwa ofisi hizo pamoja na Mtaa wa Stesheni na maeneo ya Posta ni kuwa jirani na Mahakama hiyo. Magari yalizuiwa kutembea katika njia na maeneo ya karibu na ofisi pamoja na Mahakama hiyo huku kukiwa na idadi kubwa ya askari polisi na magereza kwa muda wote wa takriban saa mbili.

AMREF YAANDAA CHAKULA CHA HISANI KUCHANGISHA FEDHA ZA KAMPENI YA “STAND UP FOR AFRICAN MOTHERS”

Image
Mkurugenzi wa Taasisi ya AMREF Tanzania Dk.Festus Ilako akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu  halfa ya chakula cha hisani ya kuchangisha fedha itakayokuwa na kauli mbiu ya “Stand for African(Tanzania) Mother’s ili kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama na watoto,halfa hiyo itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Bi.Teddy Mapunda  na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa AMREF Tanzania Dk, Rita Noronha. Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Bi.Teddy Mapunda  akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu halfa ya chakula cha hisani ya kuchangisha fedha itakayokuwa na kauli mbiu ya “Stand for African(Tanzania) Mother’s ili kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama na watoto,halfa hiyo imeandaliwa na AMREF wakishirikiana na Montage itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam. Waandishi wa Habari

WAASI WA M23 WAMUUA MWANAJESHI WETU WA JWTZ HUKO KONGO

Image
TAARIFA KUHUSU TUKIO LA KUFARIKI KWA AFISA WA JWTZ KATIKA JUKUMU LA KULINDA AMANI - DRC, GOMA 1. Kama mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO. 2. Tarehe 28 Agosti 2013 wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha majeruhi. Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri. 3. MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa marehemu. Imetolewa na: Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi. Dar es Salaam.

MFALME QABOOS ATOA MSAADA KWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Image
Na Kassim Ali na Amina Abeid (ZJMMC) Sultan Qaboos wa Oman ametoa msaada wa Riali milioni tatu na laki moja za nchi hiyo  kwa ajili ya  ujenzi wa Msikiti mkubwa  utakaojengwa katika  eneo la Chuo cha Kiislamu Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.  Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mazizini,  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamhuna amesema ujenzi  wa msikiti huo unatarajiwa kuanza  wakati wowote baada ya kutiwa saini makubaliano ya msingi kati ya Zanzibar na Oman. Amesema msikiti huo, pamoja na shughuli za ibada, pia  utakuwa  ni chimbuko la kuanzishwa Chuo Kikuu cha Kiislamu Zanzibar na kufanikisha azma ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani karume aliependekeza kujengwa Chuo Kikuu cha Kiislamu katika eneo hilo alipokifungua chuo hicho. “Maandaliz yote ya kujengwa msikiti huu yamekamilika na utakuwa na sehemu ya kusalia wanawake na wanaume, madarasa sita ya kusomea, chumba cha Kompyuta na  

RAY C AOKOKA RASIMI...HIZI NI PICHA ZAKE AKIBATIZWA

Image
  Yule dada yetu msanii maarufu wa nyimbo za bongo fleva  leo hii amewaka bayana ya kuwa yeye na shetani sasa ni paka na panya. Ray C amethibitisha hayo katika post zake za instagram. 

WAZIRI FENELLA AKUTANA NA BONDIA FRANCOIS BOTHA (WHITE BUFFALO)

Image
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akielezea kufurahiswa kwake na ukuaji wa mchezo wa ngumi hapa nchini alipokutana na  Bondia maarufu duniani na aliyewahi kuwa bingwa wa dunia mara mbili  Francois Botha (White Buffalo) kushoto jana jijini Dar es Salaa. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akiwa na  Bingwa wa duni mara mbili wa mchezo wa ngumi Bondia Francois Botha (White Buffalo)  wakipiga picha baada ya kukabidhiwa zawadi ya picha ya bondia huyo ikionyesha enzi za ujana wake jana jijini Dar es Salaam. Botha yupo nchini kufuatia kuwepo kwa pambano la ngumi la dunia litakalofanyika kesho huku likiwakutanisha mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phill William wa Marekani. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt fenella Mukangara na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara na wageni walioambatana na Botha  jana jiji

"FAMILIA IMENITENGA BAADA YA KUOA ALBINO'...MUME

Image
KIJANA aitwaye Priscus Mushi, mkazi wa Mbezi jijini Dar ambaye ni muumini wa Kanisa la Efatha linaloongozwa na Mchungaji Josephat Mwingira ameanika masikitiko yake baada ya kutengwa na baadhi ya ndugu kufuatia kuoa mlemavu wa ngozi ‘albino’ aitwaye Tumaini Murungu. Akizungumza katika Ukumbi wa Maji uliopo maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo sherehe za ndoa zilifanyika, Mushi alisema alipotangaza nia ya kumuoa Tumaini baadhi ya ndugu zake walimtenga lakini hakukata tamaa kwani aliendelea na taratibu za ndoa. “Nilimpenda sana Tumaini na niliamini ndiye mwanamke wa maisha yangu lakini nilipowaambia ndugu zangu kuwa nataka kumuoa, baadhi walinitenga kwa uamuzi wangu huo wa kumuoa Tumaini ambaye ni mlemavu wa ngozi eti nitakuwa nimeleta balaa nyumbani. “Nilimuomba Mungu anisaidie na nikaongea na waumini wenzangu ambao walikubali kunifanyia sherehe.  Nawashukuru sana wakwe zangu ambao walinipokea na kunipa ushirikiano katika kulitimiza tukio hili. Pia

Edward Lowassa asherekea kutimiza Miaka 60!

Image
HONGERA SANA MHESHIMIWA LOWASSA. Mwalimu Alikuwa Mwalimu, Atabaki Kuwa Mwalimu... Hii ilikuwa 1967. wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wakutana kutoa maoni ya rasimu ya Katiba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro(katikati) akisisitiza jambo leo juu ya maoni ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhusu rasimu ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari –MAELEZO jijini Dares Salaam na kushoto wa kwanza ni Mkurugenzi wa Idara ya hiyo, Assah Mwambene WATU 13 WAFA NA 11 MAJERUHI AJALI MBAYA MKOANI SHINYANGA

VIDEO YA UCHI YA MRISHO NGASA AKIWA NA MDOGO WAKE FLORAH MBASHA GESTI YAVUJA

Image
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka, Taifa Stars na mchezaji wa Yanga, Mrisho Ngasa, ameingia kwenye scandal nzito baada ya mkanda wake wa ngono kuvuja mtandaoni.   Mkanda huo  unamuonesha mchezaji huyo akiwa kwenye ‘suti yake ya kuzaliwa’ pamoja na msichana wakivunja amri ya sita.   Huku kukisikika muziki wa aina mbalimbali ukiwemo wa reggae, wapenzi hao wanasikika wakizungumza na kucheka wakati wakiendelea na tendo hilo.   Video  imewekwa  hapo  c hini << BOFYA  HAPA  KUIONA  VIDEO>>

BASI LA HOOD LAUA MTU MMOJA NA KUJERUHI 15

Image
Mtu mmoja amefariki dunia na 15  wamejeruhiwa baada ya basi  la Kampuni ya Hood  likitokea kilombero kwenda jijini  Dar es salaam kumgonga  mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni  Mikese Mkoani  Morogoro.    Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro  Bonifasi Mbao  akizungumza kwenye  eneo la tukio amesema chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi  gari  ilimshinda na kugonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka ambapo  dereva wa basi amekimbia mara baada ya tukio la ajali...   Taarifa za  madaktari  katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro  zimeeleza  majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu umehifahiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro . -ITV

KWELI HUU NI USHETANI KWA RIHANA ANGALIA HIZI PICHA ZAKE NDO UTAAMINI MWENYEWE

Image
HATARIIII...:

HATIMAYE AUNT EZEKIEL AFUNGUKA NA KUWEKA WAZI ISHU NZIMA YA KUSHAMBULIWA NA CHUPA AKIWA CLUB NA MDADA

Image
MWIGIZAJI wa  sinema za kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ amenusurika kupasuliwa paji la uso kwa chupa baada ya kupigwa mkononi... Usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas, mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Yvonne alimpiga Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto. Watu walioshuhudia tukio hilo wamedai  kuwa, wakati Yvonne anatekeleza ukatili huo, Aunt alikuwa amesimama na marafiki zake waliotajwa kwa jina moja moja, Sajenti na Rehema.   “Ndani ya ukumbi shoo ilikuwa ikiendelea, Aunt, Rehema na Sajenti walisimama nje, ghafla alitokea Yvonne akiwa na chupa mkononi, akailenga kwenye paji la uso la mwenzake, bahati nzuri Aunt aliiona na kukinga mkono,” kilisema chanzo. Kikaendelea: Vurugu kubwa ilizuka, ilibidi shoo ndani isimame ili kushughulia suala hilo. Aunt alikimbizwa Aga Khan, Yvonne akapelekwa msobemsobe Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo anashikiliwa. Baada ya taarifa hizo, juzi m

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI MOTO,WABUNGE WA TANZANIA WATOKA NJE KUPINGA WABUNGE WA NCHI NYINGINE KUTOKA NJE KUSHINIKIZA HOJA ZAO

Image
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA)Magreth Zziwa akimsikiliza mbunge wa bunge hilo kutoka Tanzania,Shyrose Bhanji wakati wakielekea bungeni. Spika akiongoza kikao cha leo mchana ambacho kiliahirishwa baada ya wabunge wa Tanzania kutoka nje Wabunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA)wakitoka ndani ya ukumbi wa bunge hilo leo kupinga wabunge wenzao wanaoshinikiza hoja zao kwa kutoka kwenye vikao vya bunge hali inayoshusha hadhi ya Spika,bunge na wabunge wenyewe,kutoka kushoto ni Mh.Twaha Taslima,Mh.Shyrose Bhanji,Mh.Abdula Mwinyi na Nderakindo Kessy Mbunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA)akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari yalipo makao makuu wa Afrika Mashariki jijini Arusha baada ya kutoka nje na kikao kuhairishwa hadi kesho Kiongozi  wa baraza la Wawakilishi Zanzibar,Ali Mzee(kulia)akizungumza na wabunge wa Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA)kutoka kushoto ni M

HUYU NDO JAMAA ALIEMSHIKA RIHANNA MAKALIO WAKIWA JUKWAANI AFUNGUKA UHUSIANO WAKE NA RIHANNA...!!

Image
Kufuatia rapa A$ap Rocky kuonekana katika pozi za utata na Rihanna hivi karibuni na kufikia hatua ya watu kuanza kufikiri kuwa huenda kuna kitu kimeanza kati yao, Rapa huyu ameamua kufafanua kilichokuwa kinatokea eneo la tukio. A$ap Rocky amesema kuwa hataki kujiingiza katika matatizo ya tetesi kumhusu yeye na Rihanna kwasababu hakuna kitu chochote kinachoendelea kati yao, na yeye na Rihanna ni marafiki wakubwa tu. Rapa huyu amesema kuwa anampenda Rihanna kwasababu anasapoti kazi zake na hakuna cha ziada, ingawa taarifa za chini chini zinaweka wazi kuwa, Tokea wawili hapa walipofanya tour pamoja, wamejijengea ukaribu wa ajabu ambao unazua maswali mbalimbali kila mara wanapokuwa pamoja