Manara Amuangukia Rais Karia Akili Kukosea Kama Binadamu, Aomba Yaishe

Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Sunday Manara

MSEMAJI wa Yanga Haji Manara amemuomba msamaha Rais wa TFF Wallace Karia kutokana na tukio lililotokea Jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

 

Mara baada ya mchezo huo kuna video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha Afisa huyo wa Yanga akijibizana au kutupiana maneno na Rais wa TFF Wallace Karia huku wengi wakitafsiri kuwa Manara alikuwa akimtukana Rais huyo.

 

Akiongea na waandishi wa habari Manara amenukuliwa akisema:

“Rais nimekuja kwa kukujibu vile au kujibizana mimi na wewe nimekosea “I’m Sorry” mi ni mdogo wako mimi ni kama mwanao, No matter labda wewe ndiye uliyeanza lakini kukujibu tu hata kama ulinianza nimekosea, I’m Sorry My President of Football.” Alisema Manara

Manara amemuomba msamaha Rais wa TFF Wallace Karia

Aidha Manara ametumia nafasi hiyo kuwaomba radhi mashabiki na wapenzi wa soka nchini ambao wanaona kwa kujibu vile alikosea akisema yeye ingawa amekaa kwenye masuala ya soka kwa muda mrefu lakini anabaki kuwa binadamu pia hivyo anaomba msamaha.

 

Tayari kumekuwa na mitazamo tofauti miongoni mwa wadau wa soka ambao wengine wanadai Haji Manara amekuwa na mwendelezo wa makosa ya utovu wa nidhamu hasa kwa viongozi wa mamlaka ya mpira nchini hivyo kwa hatua aliyofikia ya kujibizana na Rais wa TFF ni wazi amefikia hatua mbaya ambayo sasa anahitaji kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sharia.

Comments

Popular posts from this blog