Mmiliki Mabasi ya J4 Ahukumiwa Kifo kwa Kuwaua Wenzake

MAHAKAMA Kuu Mwanza imemhukumu adhabu ya kifo mfanyabiashara wa kampuni ya mabasi ya J4, Jumanne Mahende (45) baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kuwaua watu wawili kwa kukusudia. Jumanne alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji namba 131 ya mwaka 2015.

Anadaiwa kuwa Julai 13, mwaka 2015, saa 4 usiku, aliwaua kwa risasi, Ali Mohamed, fundi ujenzi wa Igoma wilayani Nyamagana na Claude Sikalwanda wa Nyasaka, Ilemela, Mwanza.

Kwa mujibu wa RPC Mwanza, Mkumbo alisema Saa 4 usiku Julai 13 mwaka 2015, mkurugenzi wa kampuni ya mabasi J4 Express akiwa anajiandaa kufunga ofisi yake, alikutana na watu wawili Ally Mohamed (35) na Claude Sikalwanda (35), ghafla ukaanza mzozo uliopelekea Mahende kuwapiga risasi na kufariki papo hapo.

Kwa upande wa ushahidi, mke wa marehemu Ally Mohamed, Donatha Gabriel na Aziza Sikalwanda ambae ni dada wa marehemu Claude Sikalwanda waliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 13 Julai, 2015,  siku ya tukio la mauaji lilipotokea marehemu waliwaaga kuwa wanaenda kuonana na bosi wao ambaye ni mtuhumiwa.

Inspekta Benedict Manyanda ambaye ni shahidi namba tatu katika kesi hiyo aliiambia mahakama kuwa siku ya tukio alifika eneo husika ambapo alikuta miili miwili ya marehemu ikiwa chini na baadaye kuipelekea hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Comments

Popular posts from this blog