MZEE GELARD: AGNESS ALINIAGA KABLA HAJAFA, NIKALIA!



MZEE Gerald Waya, ambaye ni baba mzazi wa aliyekuwa Msanii wa Bongo Movies na Model, Agness Gerald ‘Masogange’, amesema mwanaye alikuwa nguzo kubwa katika maisha yake, hivyo kifo chake ni pigo kubwa kwake na familia nzima.
Akizungumza nyumbani kwake, Mbalizi wilayani Mbeya, Mzee Waya alisema Masogange ni mtoto wake wa nne katika familia ya watoto sita, wa kike wakiwa ni watano ambapo ameeleza kwamba Masogange alisoma Shule ya Msingi Utengule iliyopo Mbalizi na Sekondari ya Sangu ambapo alikomea kidato cha pili baada ya kupata matatizo.
Aliishia kidato cha pili akapata matatizo, hivyo ilibidi aache shule. Tulikosana kidogo lakini tukayamaliza yeye akaenda Dar es Salaam. Agness amekuwa nguzo kwangu, alikarabati nyumba hii ninayoishi kwa sasa na nilikuwa nafarijika sana nikimuona, lakini leo kusikia msiba huu kwa kweli inaniuma sana,” alisema Mzee Waya.
Alinipigia simu tukaongea naye akaniambia ‘mimi baba ninaumwa’, nikamuuliza nini tatizo akasema, ‘baba niombee tu kwa Mungu’. Na Jumamosi iliyopita nilimpigia tena simu wakati akiwa hospitali kujua maendeleo yake lakini akaniambia ‘baba byee’. Nikaanza kulia, na hapo sikuwasiliana naye tena hadi nilipopata taarifa za kifo chake,” alisema Mzee Waya.

Comments

Popular posts from this blog