Msigwa afunguka haya Bungeni

Kamatakamata ya viongozi wa vyama vya siasa, wakiwemo wabunge leo Februari1, 2018 imemuibua bungeni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kusema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Msigwa ameibua hoja hiyo katika kipindi cha maswali na majibu, baada ya kuulizwa swali la nyongeza akihoji sababu za wanaokamatwa kushikiliwa kwa muda mrefu katika vituo vya polisi.

“Mimi ni mhanga wa jambo hili napenda kujua msingi wake ni nini, lini mambo haya yatakoma,” amesema.

Mbunge huyo amehoji lini taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu ambayo ilieleza kuhusu kamatakamata itawasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa.

Akijibu suala hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde amesema “..,  naomba wananchi wawe watulivu na kujiepusha kufanya mambo yasiyofaa.”

Amesema kwa mujibu wa Katiba, tume hiyo inapaswa kuwasilisha taarifa zake kwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya haki za binadamu.

Comments

Popular posts from this blog