BREAKING NEWS: KAMPUNI YA TTCL “YAFUTWA”

Kampuni ya Mawasiliano Tanzania ya (TTCL), sasa haipo tena, imebadilishwa na kuwa Shirika la (TTCL Corporation).

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa, amesema kuwa anamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuona wa kuwa na shirika la mawasiliano madhubuti kwa ajili ya kuleta maslahi mapana ya nchi, huku akitoa shukrani pia kwa Wabunge wote kwa kukubali kupitisha muswada huo.

Aidha Prof Mbarawa, amesema uwepo wa sheria ya shirika la mawasiliano unatoa fursa ya kuboresha sekta kwa kuweka mazingira mazuri ya usimamizi wa miundombinu ya mikakati chini ya shirika hilo.

Profesa Mbarawa pia amewajulisha Watanzania wote kuwa mabadiliko ya kuhama kutoka kampuni kuwa shirika la mawasiliano hayatawaathiri kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zinatolewa na kampuni ya simu ya (TTCL) huku akielezwa kuwa wanaodaiwa na iliyokuwa kampuni hiyo watatakiwa kulia madeni yao kama mikataba yao inavyosema na wanaoidai watalipwa pia.

Comments

Popular posts from this blog