Madereva boda boda wenye hasira wateketeza Basi kwa moto


Madereva wa Boda boda wenye hasira wameliteketeza Basi la abiria la Kampuni ya Simba  Coach lililokuwa linatokea jijini Nairobi kwenda Malindi nchini Kenya jana mchana.

Basi hilo ambalo kabla ya tukio hilo mashuhuda wamesema kuwa lilimgonga muendesha bodaboda mmoja na kufa hapo hapo lakini halikusimama kitu ambacho kilipelekea waendesha boda boda kuanza kulikimbiza.

Wakielezea tukio abiria wamesema dereva wa Basi alitaka ku-overtake gari ndogo katika eneo la Kijiwetanga na ndipo alipomgonga dereva huyo wa Boda boda.

Abiria wamesema baada ya Basi hilo kusimamishwa na madereva boda boda waliamuriwa kutoka kwenye Basi hilo kabla ya kulichoma moto.

Tayari Kamanda wa Polisi mjini Malindi,  Matawa Muchangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na dereva wa gari hilo bado anatafutwa huku Dereva wa boda boda aliyegongwa mwili wake umepelekwa katika Hospitali ya Malindi.

Chanzo:The Star Kenya

Comments

Popular posts from this blog