Mzee wa Upako kumbadili dini Q-Chief?

Msanii wa muziki wa bongo fleva Q Chief ambaye hivi karibuni ameachia ngoma yake mpya ya 'Naogopa', amezungumzia suala la kubadili dini na kuingia kwenye dini nyingine, baada ya kuwa karibu na mchungaji Anthony Lusekelo.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Q Chief amezungumzia suala hilo na kusema huwa familia yake upande wa mama ni Wakristo na ana amini katika Mungu, lakini sio rahisi kwake kubadilisha imani yake.

"Familia yangu upande wa mama wengi ni wakristo, lakini wamegawanyika kutoka kwenye uislam kwenda ukristo, baba yangu ni muislam, babu yangu ana msikiti kwa hiyo sio jambo jepesi kutoka kwenye dini yangu imani yangu kwenda kwenye imani nyingine, naamini Mungu ndiye jibu sahihi, lakini huwa nachukua ushauri wa viongozi wa dini tofauti tofauti", alisema Q Chief
Q Chief aliendelea kwa kuzungumzia kitendo chake cha kuwa karibu na Mchungaji Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako', na kusema Mchungaji huyo ni sawa na kaka yake na anapenda anavyomshauri.

"Kuna siku moja nilipigiwa simu usiku kama saa saba hivi, kupokea ni Mzee wa Upako nikashtuka, nikasema kuna kitu gani au zali zimenindondokea! lakini nikagundua ni shabiki yangu namba moja, na siku zote amekuwa akitamani kunishauri, kunijenga kiimani lakini pia kuzungumza na mimi kama kijana, kwamba lolote unalopitia usisahau Mungu amekuweka kwa sababu, na Mungu yupo kuwainua wale walioanguka, naheshimu ushauri wake kama kiongozi, kama kaka mshauri kama mchungaji", alisema Q Chief.

Comments

Popular posts from this blog