Aveva, Kaburu hali tete

Kesi inayowakabili Rais wa Simba Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange 'Kaburu' imehairishwa hadi Agosti 16 mwaka huu kutokana na kuwa upelelezi hujakamilika dhidi yao.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Victoria Nongwa ambapo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ambayo mawili kati ya hayo ni ya utakatishaji fedha.

Viongozi hao walikamatwa na TAKUKURU miezi miwili iliyopita kutoka sasa wakikabiliwa na mashitaka ya kutakatisha fedha mpaka kupelekea kunyimwa dhamana.

Comments

Popular posts from this blog