TAARIFA YA UTEUZI WA WAGOMBEA WA UJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

1.   Tarehe 17 Machi, 2017 nilitoa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali Namba 376 kuhusu Siku ya uteuzi na Siku ya Uchaguzi. Katika Tangazo hilo, nilipanga Siku ya tarehe 30 Machi, 2017, saa Kumi (10.00) Jioni kuwa Siku ya Uteuzi wa Wagombea na pia siku ya tarehe 04 Aprili, 2017 saa Tano (5.00) Asubuhi kuwa Siku ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki.

2.   Aidha, natoa shukrani zangu za dhati kwa wadau wote hususan Vyama vyote vya siasa nchini kwa ushirikiano mzuri nilioupata kutoka kwao katika zoezi zima la mchakato wa uteuzi wa wagombea.

3.   Vile vile, navipongeza na kuvishukuru vyama vyote vya siasa vyenye haki ya kushiriki uchaguzi kwa kuendesha mchakato wa uteuzi wa wagombea kwa uwazi na demokrasia kubwa.

4.   Pia navishukuru vyombo vya habari na wanahabari wote kwa ujumla kwa kuhabarisha umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa Bunge na Taifa kwa ujumla.

5.   Kipekee nawashukuru na kuwapongeza wananchi wote waliojitokeza kupitia vyama vyao kugombea katika uchaguzi huu ambapo jumla ya Watu 505 walijitokeza kugombea kupitia vyama vifuatavyo:


Comments

Popular posts from this blog