Wanafunzi 80 Mkoani Kilimanjaro Wasimamishwa Masomo kwa Ujauzito.

mimbaWANFUNZI 80 wa shule za msingi na sekondari mkoani Kilimanjaro wamesimamishwa masomo katika kipindi cha kuanzia mwezi January hadi Julai mwaka huu baada ya kubainika kuwa na ujauzito.
Afisa elimu mkoa wa Kilimanjaro Bi Euprasia Buchuma amemweleza Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia kuwa tatizo la ujauzito kwa wanafunzi mkoani Kilimanjaro ni kubwa hali ambayo inasababisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kike kushuka kila mwaka.
Amesema tatizo hilo limeonekana kubwa baada ya agizo la Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kutaka wanafunzi wakike wapime ujauzito wakati wanarudi mashuleni baada ya kumaliza likizo na kwamba muamko wa jamii kuwachukulia hatua wale wanaowabebesaha wanafunzi ujauzito ni mdogo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw.Saidi Meck Sadick amesema wilaya ya Rombo inaongoza kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi 22 wenye ujauzito ikifuatiwa na wilaya ya Siha wanafunzi 12,Hai 11 huku wilaya ya Same ikiwa haijabainika kuwa na mwanafunzi wa kike mwenye ujauzito.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amewaagiza maafisa elimu nchini kuhakiki taarifa za wanafunzi hewa na kwamba kwa wilaya au mkoa utakayobainika kuwa na wanafunzi hewa Afisa Elimu husika atawajibishwa.

Comments

Popular posts from this blog