Rais JPM Uso kwa Uso na Lowassa

Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (1)
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (3)
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa wakati wa hafla ya maadhimisho ya Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya Ndoa ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa . Kushoto ni Mama Regina Lowassa
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (4)
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mhe. Edward Lowassa wakati wa ibada ya maadhimisho hayo.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (6)
Rais Magufuli akiongea jambo na Mhe. Lowassa.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (9)
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa katika picha na Rais Magufuli na viongozi wastaafu na wana familia.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (2)
  Rais Dkt. Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwapongeza Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa.Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (7)
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipongezwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (8)
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea zawadi kutoka Parokia ya Upanga ya Mt. Imakulata.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (10)
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakikata keki.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (1)
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akitoa shukurani zake kwa wote waliohudhuria na waliofanikisha sherehe hizo.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (11)
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Maria Nyerere na Mama Shadya Karume.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (12)
 Bw. Nicholaus Mkapa akijianda kumimina champagne isiyo na kilevi  kwa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (13)
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akigongesha glasi na viongozi  wastaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM na Katibu Mkuu wake.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (2)
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (5)
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Kinana akisalimiana na Waziri mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa.
Jubilee ya miaka 50 ya Mkapa (3)
Lowassa na Kinana wakinong’onezana jambo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana alikutana uso kwa uso na aliyekuwa mpinzani wake mkubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.
Katika uchaguzi huo, Lowassa aliyekuwa akiwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) alipata zaidi ya kura milioni sita huku Rais Magufuli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akishinda kwa kupata kura zaidi ya milioni nane.
Viongozi hao walikutana katika maadhimisho ya Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya Ndoa ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa yaliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na hafla iliyofanyika nyakati za mchana katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa uliopo kando ya kanisa hilo.
Jubilei hiyo ilihudhuriwa na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais wa Rais Magufuli Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Cleopa Msuya, Dkt. Salim Ahmed Salim na Jaji Joseph Warioba.

Comments

Popular posts from this blog