NE-YO Kugonga Shoo na Nguli wa Bongo Fleva Wiki Ijayo Mwanza

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(Katikati)akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, (hawapo pichani) wakati wa kutangaza baadhi ya wanamuziki nchini ambao watatoa burudani pamoja na Mwanamuziki nguli kutoka Marekani NE-YO, katika Uwanja wa (CCM) Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka na Vodacom Festival 2016.Wengine katika picha kushoto ni Mwakilishi wa NE-YO,E.Jay Mathews na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo, Dkt. Sebastian Ndege.
Mwakilishi wa Mwanamuzi nguli toka nchini Marekani NE-YO, E.Jay Mathews (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangazwa kwa wasanii watakaotoa burudani pamoja na mwanamuziki huyo katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival 2016, litakalofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wapili (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt. Sebastian Ndege, Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, George Sozigwa Mkuu wa masuala ya ulinzi na Usalama wa tamasha hilo.

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul”Diamond Platinum’s” akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na jinsi atakavyoshiriki kutoa burudani na kuimba wimbo wa pamoja na mwanamuzi NE-YO wa nchini Marekani katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival 2016, litakalofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo, Dkt. Sebastian Ndege, Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania.



Moto wa burudani kuwashwa jijini Mwanza Jumamosi ijayo

NE-YO kushusha bonge la shoo kushirikiana na wasanii nguli wa Bongofleva nchini

Wakiwemo Diamond Platinum’s, NEY wa Mitego,Fid Q,Ruby,Baraka the Prince,Juma Nature,Mr.Blue na wengine kibao.

Pia tiketi kupatikana kupitia huduma ya M-PESA

Moto wa burudani utawaka katika jiji la Mwanza Jumamosi ya wiki ijayo ambapo msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva kutoka Marekani NE-YO atakapo shusha bonge ya shoo kwa kushirikiana na wasanii wa hapa nchini katika uwanja wa CCM Kirumba kwenye onyesho lililotayarishwa na Jembe Media chini ya Udhamini wa Vodacom Tanzania.

Akiongea juu ya onyesho hilo la kihistoria katika ukanda wa ziwa Magharibi,Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inayo furaha kudhamini tamasha hili kubwa litakaloleta burudani ya muziki kwa wateja wake na wananchi kwa ujumla.

Aliwataja baadhi ya wanamuziki watakaowasha moto kumsindikiza NE-YO kuwa ni Diamond,Ney wa Mitego,Fid Q,Ruby,Baraka the Prince,Juma Nature,Mr.Blue,Stamina,JJ Bendi na wengineo .

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo, Dkt.Sebastian Ndege aliwataka wapenzi wa muziki kujitokeza kupata budurani ya mwaka katika tamasha hilo na mipango ya tamasha hilo kubwa imekamilika na kuwataka wapenzi wa muziki wa Mkoa wa Mwanza wakae mkao wa kula wa ya karne.

Kuhusiana na viingilio alisema kuwa tiketi zitauzwa kwa shilingi elfu kumi na kuongeza kuwa wanamuziki watakaoshiriki onyesho hili wamejipanga kutoa burudani kisawasawa na kukata kiu ya wapenzi wa muziki wote Nchini.

Alisema tiketi za onyesho hilo zitauzwa katika vituo mbalimbali Nchini yakiwepo maduka ya Vodacom Tanzania,Pia zitapatikana kupitia huduma ya M-Pesa,Katika kuwapunguzia washabiki usumbufu wa kupanga misururu ya kununua tiketi za onyesho hilo pia zitauzwa kwa kupitia huduma ya M-Pesa bila kuwepo na makato yoyote ya kutumia huduma hiyo ambapo watakaonunua tiketi kwa huduma hiyo kutakuwepo na utaratibu maalumu wa kuingia kwenye onyesho cha muhimu ni kutunza namba zao za kumbukumbu ya mhamala wa malipo.Jinsi ya kujipatia tiketi kwa njia ya M-PESA mteja anatakiwa kupiga *150*00# na kuchagua LIPA KWA M-PESA
Chagua MANUNUZI
Chagua JEMBEKA FESTIVAL
Weka namba ya kumbukumbu – 200200
Weka kiasi – 10,000
Weka Namba yako ya siri na kwa wale wa tiketi za VIP namba ya kumbukumbu ni 200100 bila malipo yeyote yale.
CREDIT:GPL

Comments

Popular posts from this blog