Malaika afunguka ‘kinachopukutisha’ mwili wake


DSC_0026
MWANAMUZIKI mrembo anayetamba na Wimbo wa Raruaraua, Malaika Exavery amefungukia kinachoupukutisha mwili wake kuwa siyo ugonjwa kama watu wanavyodhani bali ameamua kupungua tu kwa kula kabichi na parachichi.
 Akizungumza na Amani Malaika alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakimhoji kupungua kwa mwili wake huku wengine wakijua ni tatizo la kiafya ambalo lilimpata.
“Kilichonipunguza haraka ni kula kabichi, parachichi na maji mengi na wala siyo tatizo la ugonjwa kama wengi wanavyodhani.
“Nimekuwa nikishindia kabichi ya kuchemsha, parachichi kisha nashushia na maji na ndicho kilichonifanya kupungua kilo zaidi ya saba sasa,” alisema Malaika ambaye kadiri siku zinavyokwenda anazidi kujikusanyia mashabiki kibao

Comments

Popular posts from this blog