BREAKING NEWZ:Mke wa Mwai Kibaki Afariki Dunia.

Lucy-Kibaki-2
NAIROBI, KENYA
Mke wa rais wa zamani nchini Kenya, Mwai Kibaki, Mama Lucy Kibaki amefariki dunia leo asubuhi, Jumanne, Aprili 26, 2016 akiwa kwenye matibabu mjini London Uingereza.
Taarifa iliyotolewa na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta imesema, Mama Lucy Kibaki amefariki akiwa katika hospitali ya Bupa Cromwell mjini London Uingereza alikokuwa akitibiwa.
Mwezi mmoja uliopita, Mama Lucy alipewa rufaa ya kwenda Nairobi Hospital akitokea hospitali ya Gertrudeiliyopo Muthaiga, baada ya hali yake kutokuimarika wiki iliyopita alisafrishwa hadi mjini Landon kwa matibabu ambako ndiko mauti yamemkuta.
Akithibitisha kifo hicho, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa kenya imesikitishwa na kifo cha mama Lucy mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki. Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari Uhuru amesema Mama Lucy amekuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Amesema kuwa Kenya imempoteza mwanamke aliyechangia mengi katika maendeleo ya taifa la Kenya hususan katika vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi. Rais ametuma risala za rambi rambi kwa mtangulizi wake Mwai Kibaki pamoja na familia yake.
Uhuru-Kenyattas-press-release

Comments

Popular posts from this blog