BOSI WA ZAMANI WA TRA HARRY KITILLYA, SHOSE SINARE NA SIOI SOLOMONI WANYIMWA DHAMANA

Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya, akipunga mkono kwa baadhi ya wanahabari waliokuwepo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam leo.


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imepuuza ombi la dhamana ya kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni ambapo wamerejeshwa rumande.
Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.
Dhamana yao imesikilizwa mbele ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu ambapo mawakili wa pande zote mbili waliwasilisha hoja zao.
Dk. Lingo Tenga ndiye aliyeongoza jopo la mawakili upande wa watetezi ambapo upande wa serikali umesimamiwa na Oswadi Tibabyekonya, Wakili Mkuu wa Serikali Mahakama ya Kisutu.

Upande wa utetezi uliomba mahakama kubatilisha mashitaka ya utakatishaji pesa haramu uliosababisha watuhumiwa hao kukosa dhamana. Tibabyekonya ameieleza mahakama kuwa, shitaka la utakatishaji fedha halina dhamana.


Upande wa utetezi ulifanya mapitio ya kesi mbalimbali zinazofanana na kesi hizo ikiwemo kesi namba 314 ya mwaka 2015 kwenye Mahakama ya Rufaa ya Mwanza iliyokuwa ikimkabili Kigunda Francis aliyeshitakiwa kwa kosa kama hilo lakini alipewa dhamana.

Christopher Msigwa, wakili wa serikali amesema kuwa kesi hiyo haina dhamana kwa sababu, kosa hilo linaathiri uchumi wa taifa.

Washitakiwa wamekosa dhamana na wamerudishwa rumande hadi tarehe 22 Aprili mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mmoja wa watuhumiwa katika kesi ya kutakatisha fedha kiasi cha Dola milioni sita za Marekani, Shose Sinare akisindikizwa na Askari wa Jeshi la Magereza kwenda kwenye gari maalum, tayari kwa safari ya kurudishwa rumande baada ya kesho yao kusogezwa mbele.
Sioi Solomoni akijiangaa kupanga Gari hilo.


Comments

Popular posts from this blog