MBARAWA AFUNGUA RASMI SAFARI ZA TRENI RELI YA KATI

Muonekano wa Sehemu ya Reli katika eneo la Kidete, Wilayani Kilosa, mara baada ya ukarabati kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kukata Mawasiliano kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Kazi za ukarabati wa mwisho zikiendelea katika eneo la Kidete, Wilayani Kilosa, mara baada ya ukarabati kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kukata Mawasiliano kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Treni ya Mizigo ikiwa tayari kuanza safari katika eneo la Kidete Wilayani Kilosa, kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa eneo hilo, uliodumu kwa takriban miezi miwili na hivyo kurudisha mawasiliano ya reli kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Mhandisi Felix Nlalio, kuhusu namna ya kudhibiti mkondo wa maji katika mto mkondoa yasiathiri hifadhi ya reli.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akikagua bwawa la Kidete linaloelezwa kuathiri hifadhi ya reli katika stesheni za Mzaganza, Munisagara, Kidete na Magulu Wilayani Kilosa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa viongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), kuhusu namna ya kushirikisha wananchi kulinda hifadhi ya reli.

Comments

Popular posts from this blog