LIVE KUTOKA ZANZIBAR MDA HUU.... VIKOSI VYA 'JESHI' VYAIMARISHA ULINZI KWENYE VITUO VYA KUPIGIA KURA



07:50 Safari zote za meli kati ya bandari ya Dar es Salaam na visiwa vya Zanzibar zimekatizwa.
Hapa chini ni tangazo la kuwapasha wateja wa Azam Sealink kwamba hakutakuwa na safari za meli kuanzia tarehe 18 hadi 22 Machi kutokana na uchaguzi unaoendelea Zanzibar.




Licha ya kukatizwa kwa safari, badi wapo watu waliojitokeza wakitarajia kusafiri. Wengi wa waliofika ni wageni kutoka Ulaya ambao hawakuwa na habari.




07:44 Usalama umeimarishwa visiwani. Hapa chini ni maafisa wa usalama wakiwa na mbwa wa kunusa kabla ya Dkt Shein kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Unguja.




07:42 Baadhi ya wapiga kura wakitafuta majina yao kituoni Madungu Chake-Chake, kisiwani Pemba.




07:30 Mwanamke akipakwa wino kwenye kidole chake baada ya kupiga kura kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba.




Baadaye, atabasamu baada kutoka nje ya ukumbi.




07:20 Hii hapa ni picha nyingine ya Dkt Ali Shein, mgombea urais wa CCM baada yake kupiga kura Unguja.




07:05 Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein amepiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera katika kisiwa cha Unguja.



Shein
Image captionDkt Shein akioneasha wino kwenye kidole chake

07:00 Vituo vingi vya kupigia kura vimefunguliwa.
06:50 Maafisa wa uchaguzi wanajiandaa kufungua vituo. Vituo vinafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi alasiri.




06:40 Wapiga kura kituo cha Bungi, Unguja wasubiri kituo kifunguliwe.




06:35 Katika vituo vingi, wapiga kura hajawafika. Lakini maafisa wa tume tayari wamo vituoni pamoja na maafisa wa usalama. Hata ni kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba.




06:30 Hujambo! Wapiga kura visiwani Zanzibar wanashiriki uchaguzi wa marudio leo baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika 25 Oktoba mwaka jana kufutwa na tume ya uchaguzi. Chama cha CUF kinasusia uchaguzi huo.
Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi huo.

Comments

Popular posts from this blog