LINAH: NAJUTA KUMUANIKA MPENZI WANGU

 
STAA wa Muziki wa Kizazi Kipya, Estelina Sanga ‘Ndege Mnana’ amefunguka ya moyoni kuwa, kamwe hawezi kurudia kosa la kumuanika mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii au kwa watu na kukiri kuwa ndiyo sababu kubwa iliyochangia kuachana na mpenzi wake, William Bugeme.
Akizungumza na Showbiz kwa hisia kali msanii huyo anayebamba na Ngoma ya No Stress alisema, hakuwa akijua kama kuanika uhusiano wake kwenye mitandao ya kijamii kutamletea majanga.
“Mimi tena kumuonesha mpenzi wangu nimekoma, najutaaa! Maana kwanza wakimjua wengine watajipendekeza na kumchukua na wengine watampelekea maneno ili tugombane  hivyo bora nikae kimya labda wamjue siku ya harusi tu nimejifunza,” alisema Linah.

Comments

Popular posts from this blog