Fahamu: Osama aliacha dola milioni 29 kufadhili Jihad



Kiongozi wa kidini wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda Osama Bin Laden aliacha urathi wa dola milioni 29 kufadhili Jihad alipouawa mwaka 2011. Hayo ni kwa mujibu wa wasia wake iliofichuliwa leo.
Aliihimiza familia yake kuheshimu waysia wake na kuwashauri ''watumie mali yake yote kuendeleza jihad'' Mali yake na wasia wake ni miongoni mwa maelfu ya stakabadhi muhimu zilizofichuliwa hii leo na maafisa wa Marekani.
Aidha Bin Laden alimtaka babake amtunzie mke na wanawe endapo ataaga dunia. Kiongozi huyo wa mtandao wa kijihad wa Al Qaeda aliuawa na majeshi ya Marekani mwaka wa 2011 katika shambulizi la kufumania lililotekelezwa ndani ya Pakistan.

source:rahatupu.us

Comments

Popular posts from this blog