SPIKA WA BUNGE AENDA KUMFARIJI MAMA MARIA NYERERE

ndu1

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiweka saini kitabu cha maombolezo  alipokwenda kutoa pole Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kufiwa na mkwewe Leticia Nyerere leo tarehe 13 Januari Msasani jijini Dar es Salaam.
ndu2
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimfariji Bi. Rose Nyerere binti wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipokwenda kuwafariji kufuatia kuondokewa na Mpedwa wao Leticia Nyerere.
ndu3
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsalimia Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipokwenda nyumbani kwake kumpa pole kufuatia kifo cha mkwewe wake Leticia Nyerere.
ndu4
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (aliyekaa katikati) wakati alipokwenda kumpa pole kufuatia kifo cha mkwewe wake Leticia Nyerere. Aliyekaa kulia ni Mmoja wa Wasemaji wafamilia Bw. John Shibuda.
ndu5
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na  Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati alipokwenda kumpa pole kufuatia kifo cha mkwewe wake Leticia Nyerere. Aliyekaa kushoto ni Bi. Rose Nyerere.
ndu6
Spika wa Bunge akiwa na wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akiwemo Mama Maria alipokwenda kuwafariji kufuatia kifo cha mpedwa wao Leticia Nyerere.
ndu7
Spika wa Bunge akiwa  katika picha ya pamoja na wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akiwemo Mama Maria alipokwenda kuwafariji kufuatia kifo cha mpedwa wao Leticia Nyerere.
ndu8
Spika wa Bunge akisalimia familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipokwenda kuwafariji kufuatia kifo cha mpedwa wao Leticia Nyerere.
(Picha na Ofisi ya Bunge)

Comments

Popular posts from this blog