NYUMBA YA MCHUNGAJI RWAKATARE YASABABISHA WAZIRI JANUARY KUCHUKUA HATUA HIZI KALI KWA MAOFISA HAWA



SAKATA la maofisa watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), waliosimamishwa kazi kwa tuhuma ya kukiuka miiko yao ya kazi, limechukua sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, kuagiza wafikishwe mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Pamoja na hayo, Waziri huyo amemsimamisha kazi aliyekuwa mwanasheria wa baraza hilo, John Mnyele kwa matumizi mabaya ya ofisi.
Akizungumza  jana, alisema tayari amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kuwasilisha mashtaka yanayowakabili maofisa hao watatu Takukuru kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi, ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Maofisa waliosimamishwa kazi kutokana na udhaifu huo ni pamoja na Ofisa Mazingira Mwandamizi Dk Eladius Makene, Mwanasheria Daraja la II Wakili Heche Suguta Manchare ; na Ofisa Mazingira Boniface Benedict Kyaruzi. Wanatuhumiwa kukiuka miiko ya kazi yao katika kusimamia kiwanda cha kusindika minofu ya punda kilichopo mkoani Dodoma.
Pamoja na maofisa hao, pia Mwanasheria Mnyele, anayetuhumiwa kuingia mkataba na Mchungaji Getrude Rwakatare wa kuondoa kesi mahakamani kwa niaba ya NEMC bila kuijulisha ofisi, naye anachunguzwa na taasisi hiyo ya rushwa.
Mama Rwakatare kwa sasa ana kesi mahakamani dhidi ya baraza hilo ya kupinga kubomolewa kwa nyumba yake, inayodaiwa kujengwa mahali pasiporuhusiwa.
Kiwanda hicho cha minofu ya Punda cha China, kilianza kazi hiyo rasmi mwaka 2012 huko Dodoma ambapo pamoja na kuchinja, pia huuza nyama hiyo nje ya nchi, hususan China.
Kiwanda hicho kilipatiwa vibali vyote, ikiwemo cha Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) na cha Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi cha kuchinjia.
Pia, kilikuwa na vibali vingine vya Manispaa. Hata hivyo, hakikuwa na kibali cha masuala ya mazingira kutoka NEMC.
Katika ukaguzi uliofanywa siku za nyuma na Baraza hilo, ilibainika kuwa kiwanda hicho hakina kibali hicho cha mazingira, lakini pia kilikuwa kikilalamikiwa na wananchi wanaokizunguka kutokana na kutofuata taratibu za utunzaji wa mazingira.
NEMC ilibaini kuwa kiwanda hicho, hakikuwa na mfumo wa majitaka, lakini pia kilikuwa kikichoma mabaki yanayotumika kuchinjia ndani ya kiwanda hicho na moshi wake kusambaa maeneo yanayokizunguka.
Kutokana na makosa hayo, baraza hilo lilikifungia kiwanda hicho kama adhabu na kukilipisha faini ya Sh milioni 240.
Juzi Waziri January pamoja na kuwasimamisha maofisa hao watatu kwa kukiuka miiko yao ya kazi, pia aliagiza Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo, Mhandisi Bonaventura Baya, apewe barua ya onyo kali na la mwisho kwa tuhuma za udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa baraza hilo, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa baraza hilo.

Comments

Popular posts from this blog