SHAMSA: BORA NIFE KULIKO KURUDIANA NA MUME WANGU

Imelda Mtema
MAKUBWA!! Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford ameibuka na kukataa katakata kurudiana na aliyekuwa mumewe, Dickson Matoke ‘Dick’ akisema kuwa kama watarudiana basi atakuwa ameshafariki dunia au bora afe kuliko kurudiana naye.
Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford.
Shamsa aliyasema hayo juzikati baada ya kuulizwa na Amani kama ana mpango wa kurudiana na mumewe huyo ambapo alisema licha ya kuzaa mtoto mmoja (Terry) na mwanaume huyo, lakini katika maisha yake hafikirii kamwe kurudiana naye huku akasisitiza kuwa, kwa sasa ana maisha yake mengine.
“Mimi nirudiane na Dick? Labda niwe nimekufa na ni bora nife kuliko kurudiana na Dick. Ujue sasa hivi nina thamani kubwa zaidi na nipo na mtu ambaye ananipenda, nampenda,” alisema Shamsa.Hivi karibuni, Dick aliripotiwa na gazeti moja la Global akisema bado anampenda sana Shamsha na yuko tayari kurudiana naye baada ya kumwagana.

Comments

Popular posts from this blog