HATIMAYE UKWELI KUHUSU CHUKI YA ZITTO KWA MSICHANA MSOMI DR. TULIA YATAJWA KUMBE KUNA MENGI NYUMA YA PAZIA



Jamii ya wanazuoni imekuwa ikijiuliza ni kwanini mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe anampiga vita mgombea unaibu spika Dk.Tulia Ackson.
Wanahoji ni kwanini Zitto Kabwe anamhofia huyu mwanamama wakati ana vigezo vyote vinavyompa "credibility" ya kugombea.Imefikia hatua Zitto anamnadi Mussa Azzan ambaye ni mbunge wa Ccm na kusahau kuwa yeye ni mpinzani ndani na nje ya bunge.
Hapa ndipo dhana ya usaliti kwa Zitto Kabwe inapozidi kumea kwenye masikio ya watanzania.Zitto Kabwe hataki kukubali kuwa siasa ya bunge sio yake peke yake. Mnakumbuka sakata la aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC ambaye PAC ikiongozwa na Zitto Kabwe iliamuru akamatwe na kuwasilishwa polisi!?Tena kwa makosa ambayo PAC ilikuja kuangukia pua!!
Namzungumzia Andilile Mwainyekule.Huyu ni mume wa ndoa wa Dk.Tulia Ackson.Zitto Kabwe anauona ugumu wa yeye kuiyumbisha serikali kwa skendo za kupika kama kiti kitasimamiwa na Dk.Tulia Ackson.
Zitto Kabwe anahofia Dk.Tulia Ackson kutumia mwanya wa kujua kwa undani sakata la TPDC na kuiokoa serikali na hoja ambazo Zitto Kabwe anategemea kuziibua na kuziendeleza.
Suala hapa sio unaibu spika bali ni maslahi ya mifuko ya Zitto Kabwe na hatma ya maisha yake ya kisiasa.

Comments

Popular posts from this blog