WANAHITAJIKA VIJANA 120 KUJAZA NAFASI ZIFUATAZO ZA AJIRA SERIKALINI



OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/H/67
15 Septemba, 2015
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa

mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo
hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi
zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya waajiri
mbalimbali Serikalini anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa
kujaza nafasi 120 za kazi kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
2
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xi. Mwisho wa maombi ni tarehe 29 Septemba, 2015
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa
Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya
ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
xiv. MUHIMU: KUMBUKA KUWEKA (ATTACH) BARUA YAKO YA
MAOMBI. ANUANI YA BARUA HIYO IELEKEZWE KWA KATIBU,
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA S.L.P 63100 DAR ES SALAAM.
1.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE OFFICER
GRADE II) – NAFASI 20
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika
kata na atashughulikia masuala yote ya kata
· Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbal.i ya uzalishaji,
mali, kuondoa njaa na Umasikini.
3
· Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na
Mtaa.
· Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata
yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika
Kata.
· Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo
lake.
· Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katikangazi ya
Kata.
· Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na
nakala kwa Katibu Tarafa.
· Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa
vjiji, na NGO’S katika kata yake.
· Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji,
vitongoji, na kata yake.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya Juu katika fani ya Utawala, (Public
Administration and Local Gorvernment), Rasiliamaliwatu, Sheria, Elimu ya Jamii,
Maendeleo
ya
Jamii,
Usimamizi
wa
Fedha,
Uchumi
na
Mipango
kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D. kwa
mwezi.
2.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III (WARD EXECUTIVE OFFICER
GRADE III) – NAFASI 27
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika
kata na atashughulikia masuala yote ya kata
· Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji,
mali, kuondoa njaa na Umasikini.
· Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na
vitongoji.
· Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata
yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika
Kata.
4
· Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo
lake.
· Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya
Kata.
· Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na
nakala kwa Katibu Tarafa.
· Atakuwa mwenyekiti katika vikao vya vinavyowahusisha wataalamu na watendaji
wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.
· Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji,
vitongoji, na kata yake.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
· Kuajiriwa aliyehitimu kidato cha nne au sita na mwenye Cheti cha Mafunzo ya
Stashahada katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Maendeleo ya Jamii,
Usimamizi wa Fedha, Uchumi na Mipango, kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa
Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi.
3.0 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA III (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS)
– NAFASI 20
3.1 MAJUKUMU YA KAZI.
· Kushirikiana na wakulima kuendesha mashamba ya majaribio na mashamba
darasa,
· Kutembelea wakulima/vikundi vya wakulima katika mashamba yao na kutoa
ushauri wa kitaalamu juu ya mbinu bora na za kisasa za kilimo cha kibiashara,
· Kufundisha na kuelekeza wakulima juu ya matumizi bora ya mbolea, madawa na
zana za kilimo,
· Kukusanya na kutunza takwimu za hali ya kilimo katika kijiji,
· Kubuni na kuandaa vihenge vya kisasa vya hifadhi ya mazao na kutoa elimu ya
matumizi sahihi ya mazao,
· Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo visumbufu vya mimea na mazao,
· Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika kutekeleza majukumu yake ya kila
siku,
· Kushiriki katika mchakato wa kuibua fursa na vikwazo vya maendeleo
(Opportunities and Obstacles for Development (O & OD) na kuandaa mpango wa
maendeleo ya kilimo wa kijiji (Village Agricultural Development Plan (VADP), na
· Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi kuiwasilisha kwa Afisa Ugani wa
Kata na nakala kuiwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji.
5
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne wenye Astashahada (Cheti) ya Kilimo
kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
3.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B Kwa
4.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 45
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa
Uhamiaji.
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori
· Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya
uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji
matengenezo,
· Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
· Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C”
ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua
miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi
Daraja la II.
4.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS A kwa mwezi.
5.0 MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 8
Nafasi hii ni Kwa ajili ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa
Uhamiaji.
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.
· Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia
ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.
· Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.
· Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.
· Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.
· Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi (Appointment) au
wamepata idhni ya maafisa husika.
· Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.
· Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
6
· Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa
kwenda nje.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili
na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
5.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Comments

Popular posts from this blog