James Mbatia Kuhamia Chadema...NCCR Mageuzi Wadai Amekuwa Msemaji wa Chadema Badala ya Kujenga Chama

Mbatia na Lissu
Kuna kila dalili kuonyesha mbatia atakihama chama chake kwenda Chadema. karibuni akionekana kua msemaji wa mambo ya Chadema hadi kuwashangaza wafuatiliaji wa mambo ya siasa. sasa amejitenga na viongozi wenzake wa NCCR Mageuzi hadi wanatishia kujitoa UKAWA.. ameshindwa kutetea maslahi ya NCCR ndani ya UKAWA na inaekekea amelewa mahaba ya Lowassa mtu anayedaiwa kua tajiri sana. Je Mbatia naye atakua nyumbu kufuata malisho Chadema? si siku nyingi tutapata jibu.
Sumaye ambanae inasemekana amejiunga na NCCR japo hakuna ushahidi wa kukabidhiwa kadi ameoneka na jezi ya CHADEMA kwenye mikutano akipiga debe kwa Lowassa. ni wazi NCCR ni mwathirika wa UKAWA na itabaki na ukiwa. inaelekea nyumbu wote watafuata alipo EL. alipo Edo nyumbu wote wapo. tuombe mungu apishilie mbali UKAWA kutwa uongozi ama sivyo tutaona mparurano wa kugombea vyeo.. Sumaye tayari amapewa uwaziri mkuu mbowe inasemekana atakabidhiwa hazina! mbatia bado haifahamiki etc

By Kmbwembwe

Comments

Popular posts from this blog