Hivindivyo Watu Mbali Mbali Walivyosema Huko Facebook Baada ya Hotuba ya DR Slaa Leo

'Chadema kama chama kilichokomaa na kinachojiandaa kushika dola hakina haja wala sababu ya kumjibu Dr. Wilbrod Slaa. Machungu yake tunayatambua ila kwasasa hatuna jinsi ni lazima tusonge mbele kuitoa hii nchi kwenye umasikini. Juhudi na kazi zake katika Chadema tunayatambua, tunaziheshimu na tutazienzi. Kwaheri Dr. Wilbrod Slaa ' By Renatus Kyakalaba


"Sitashangaaa kuona akili ndogo wakianza kumtukana Dr.Slaa,,,baada ya hii hotuba yake inayoweka Black and White Out,,,,,"  By Baraka Samson Chipanjilo


'Sikuwahi mpinga Dr huyu toka nianze kumuona kwenye siasa, Leo kwa mara ya kwanza nimelisikia neno rahisi sana LA kuwa ukawa wanabeba watu kwenye malori na mabasi, cheap statement! Hili nakupinga Hakuna aliyefika uwanjani usiku huo uliosema ila kulikuwa na walinzi wa jukwaa na vyombo kulikuwa na daladala mbili zilikodiwa na wafuasi kwa mapenzi yao, Dr please mdomo usiuruhusu useme yote maneno yana kawaida ya kama yakiwa marefu sana huwa baadhi yanakuelezea wewe mwenyewe ni mtu wa namna gani' By Mtonya Mgaya


'Kuuliza sio ujinga lakini. Ni kipimo cha hekima. Wacha niulize.
Zile gharama za press conference pale Serena nani kazibeba?
Nnachojua live coverage ya TV kwa lisaa na nusu si chini ya Shilingi Milioni 20 kwa TV Moja. Na pale zilikua kama TV station 4.
Ukumbi ule kwa muda wote ule si chini ya Milioni 5 mpaka 10 a kitanzania.
Swali langu nani kalipia gharama zote hizo? Nauliza tu' By Alexander Wenceslaus


'Kweli nimeamin kwenye safari ya ukombozi kuna makundi matatu
1.Kundi la waoga wa kupambana na mfumo kandamizi
2.Kundi la mamluki waliopandikizwa na wale wanaokandamiza na hawapendi mabadiliko.
3.Kundi la wapambanaji ambao wanajitolea kupambana na wako radhi kuzimwaga damu zao.
Ok nimeisikia hotuba ya Mh Slaa ila nikireflect na issue ya Lipumba nakuwa na wasiwasi na hawa watu' By Godfrey Muhimil 

Comments

Popular posts from this blog