ANASWA NA KOMBATI ZA KOMANDOO

KOMBATI (1)-001
Kijana Zakaria Joseph akiwa amevalia kombati za jeshi.
Na Haruni Sanchawa
KIJANA aitwaye Zakaria Joseph 22, (pichani)mkazi wa Maili Moja, Kibaha, mkoani Pwani, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuvaa sare za Jeshi la Wananchi waTanzania (JWTZ), huku akitaka kuzitumia kuwashawishi polisi kutoa dhamana kwa mtu mmoja (jina limehifadhiwa).
KOMBATI (2)-001 Taarifa zilizonaswa na gazeti hili zinasema kuwa, kijana huyo amekuwa akizutumia sare hizo kwa matukio tofauti huku akijifanya ni mwajiriwa wa jeshi hilo.
Katika utetezi wake mbele ya askari polisi, Zakaria alikiri kuwa sare hizo si zake na…
KOMBATI (1)-001
Kijana Zakaria Joseph akiwa amevalia kombati za jeshi.
Na Haruni Sanchawa
KIJANA aitwaye Zakaria Joseph 22, (pichani)mkazi wa Maili Moja, Kibaha, mkoani Pwani, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuvaa sare za Jeshi la Wananchi waTanzania (JWTZ), huku akitaka kuzitumia kuwashawishi polisi kutoa dhamana kwa mtu mmoja (jina limehifadhiwa).
KOMBATI (2)-001Taarifa zilizonaswa na gazeti hili zinasema kuwa, kijana huyo amekuwa akizutumia sare hizo kwa matukio tofauti huku akijifanya ni mwajiriwa wa jeshi hilo.
Katika utetezi wake mbele ya askari polisi, Zakaria alikiri kuwa sare hizo si zake na kwamba ni za kaka yake aliyetajwa kwa jina la Anord William ambaye alidai ni mfanyakazi wa jeshi hilo kikosi cha Komandoo, Morogoro.
Taarifa kutoka vyanzo vyetu zinasema kuwa mtu huyo alikamatwa katika Kituo cha Polisi  Chang’ombe, Mkoa wa Kipolisi Temeke wakati akijaribu kutumia sare hizo kuwashawishi askari hao wakubalia kumpa dhamana mtu aliyetaka kumdhamini.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa kijana huyo aligundulika kirahisi kuwa si askari kutokana na vitendo vyake kuanzia kutembea  hata kutoa salamu za kijeshi alishindwa.
Taarifa zinadai kuwa kijana huyo alipofika kituoni hapo alionekana kutokuwa na muonekano wa kiuaskari kwani alikuwa hajui taratibu za kijeshi kama vile  kutambua nani anapaswa kupewa saluti au ‘kumkaukia’ hali iliyowashangaza askari kituoni hapo na kulazimika kumhoji ili kubaini ukweli.
Aidha, chanzo hicho kilisema  kutokana na tukio hilo, mtuhumiwa  huyo amehifadhiwa eneo maalum kwa ajili ya mahojiano zaidi huku taratibu zingine  zikifanywa ikiwa ni pamoja na makachero kwenda  Morogoro Kikosi cha Komando kuthibitisha kama askari aliyetajwa na kijana huyo yupo katika kikosi hicho na kujua ilikuwaje sare zake zikawa kwa mtuhumiwa.

Comments

Popular posts from this blog