WANAWAKE WENGI HULIA NA KUUMIA SANA PALE WANAPOSHINDWA KUSHIKA MIMBA, ZIFAHAMU SABABU ZA TATIZO HILI HAPA

Miongoni mwa matatizo ambayo yanapatikana sana kwa sasa katika jamii zetu na kusababisha wanandoa wengi au wanawake wengi kukosa furaha, hili suala la kukosa uwezo wa kupata ujauzito kwa mwanamke.

Lakini kimsingi tatizo hili si swala la mwanamke pekee yake kama jamii inavyolichukulia bali ni tatizo ambalo  linahusisha pande zote mbili, yaani upande wa mwanamke na pia upande wa mwanamme, wote wawili wanapokuwa katika afya nzuri ndipo ujauzito unaweza kupatikana kwa mwanamke.

Miongoni mwa sababu zinazoweza kumfanya mwanamke ashindwe kupata ujauzito ni kama zifuatazo:

Kuziba kwa mirija (fallopian tubes), mwanamke anapokuwa na hali hii huchangia mbegu za kiume (sperms) kushindwa kulifikia yai na kulirutubisha ili ujauzito utungwe.

Kuziba kwa mirija huweza kusababishwa na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mara nyingi wanawake ambao mirija yao imeziba, hawahisi dalili zozote.



Uvimbe katika kizazi (fibroids),  hali hii nayo huchangia mwanamke kutopata ujauzito. Uvimbe huu ambao hutokea katika kuta za mji wa mimba, hivyo huweza kuzuia yai lililorutubishwa lisikae sehemu yake na hivyo kuathiri kizazi.

Matatizo katika homoni, hii ni kutokana na kwamba, mzunguko ifahamike kuwa katika mwili wa mwanamke hutawaliwa na hizi kemikali asilia ndani ya mwili ambapo mabadiliko madogo yakitokea katika uzalishaji wa hizi homoni au homoni hizo kuzalishwa wakati ambao siyo muafaka huweza kupelekea mwanamke akashindwa kupata ujauzito.

Ishu ya umri nayo kuna wakati huweza kuwa sababu kwani kadri umri  wa mwanamke unavyoongezeka, pia uzalishaji wa homoni hupungua. Kuanzia miaka 35 na kuendelea huwa kunakuwa na tatizo la kushindwa kupata ujauzito kwa wanawake wengi. (si wote ni baadhi yao)
Hizo ni baadhi tu ya sababu ambaazo huweza kuchangia mwanamke kushindwa kushika ujauzito, lakini kama wewe umekuwa na shida ya kutopata mtoto kwa muda mrefu wasiliana nasi sasa tukusaidia kwa kutumia dawa zetu za asili ili uweze kupata mtoto.

Comments

Popular posts from this blog