Asasambua mchana kweupe kumkomesha mchepuko

15825youngcoupleinlove1920x1200photographywallpaper.jpg
MUME wa mtu sumu! Kitendo cha wanawake kutembea na waume za watu ni cha kawaida kabisa katika maeneo mengi nchini na wengi wamejikuta wakikutana na balaa, lakini tabia hiyo inaendelea kila kukicha. Samora Abdallah (pichani), Afisa Mtendaji wa Mtongani, Kata ya Mbuyuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam, anao mkasa wa kusisimua ambao ni moja kati ya kesi nyingi alizopata kuzifanyia kazi ofisini kwake kama anavyosimulia;
“Hata sijui nianzie wapi, kuna siku kundi la watu walifika ofisini kwangu, nilipohoji ujio huo kwa kuwa haukuwa wa amani, nikajibiwa kwa kuoneshwa kidole kwa dada mmoja aliyeshukiwa kuchukua mume wa mwenzie. Mara wakaanza kurushiana maneno machafu, nusura wakunjane, nikawazuia na kutaka kujua kulikoni.
“Dada mmoja akaniambia kuwa binti aliyekuwa mbele yetu, anatembea na mumewe kwamba siku hiyo aliichukua namba yake kutoka kwenye simu ya mume wake na kuanza kuchat naye akijifanya ndiye yeye. Alizungumza naye mambo mengi na mwishowe akamtaka aje sehemu wakutane, dada huyo bila kujua kuwa anaingia mtegoni, akaenda.
“Baada ya kufika alipo, akakutana naye, akamuuliza alichokifuata eneo hilo, huyo mwanadada akaanza kujiumauma, akidai kuna mtu anamsubiri, basi akampigia simu yake, akasogea pembeni ili akazungumze, huyo dada mwenye mume akakata simu, akamfuata na kumzaba vibao, akimwambia yeye ndiye aliyempigia na kumuuliza kwa nini anatembea na mume wake.
“Akasema watu waliwakuta wakizozana, wakawashauri kuja ofisini kwangu, wakiwa hapa ndipo yule dada akaanza kuvua nguo ili kati yao aonekane mzuri ni nani ndipo nilimzuia na kumwambia kufanya vile ilikuwa ni kujidhalilisha, yule dada alimuomba msamaha kwamba asingerudia kutoka na mumewe aliyemdanganya.
Kama una kituko kilichowahi kukutokea ukiwa ofisini wasiliana nasi kupitia namba iliyopo hapo juu. Angalizo ni lazima uwe Mwenyekiti, Mtendaji au Mjumbe wa Shina, Kijiji au Mtaa

Comments

Popular posts from this blog