BREAKING NEWZZ......MSANII ALI KIBA AVAMIWA NA NA MAJAMBAZI NYUMBANI KWAKE KUNDUCHI

https://igcdn-photos-f-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xap1/t51.2885-15/11201793_752299184896709_1731970059_n.jpg

Hivi punde tumepokea habari ya kusikitisha na kushtusha, msanii wa Bongo Fleva @officialalikiba usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam, alivamiwa na kundi la watu wapatao 20 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi. Watu hao waliokuwa na silaha za aina tofauti yakiwemo mapanga, visu na silaha za moto walifanikiwa kuvunja kuingia ndani na kuwadhuru baadhi ya ndugu wa Alikiba na kuiba mali na kila kitu ambacho waliweza kubeba, walimpiga na kumtesa mlinzi wa nyumba hiyo wakimtaka awaonyeshe alipo Alikiba, hata hivyo hawakufanikiwa kumpata na wakaondoka muda mfupi kabla ya polisi hawajafika nyumbani kwa staa huyo baada ya kupigiwa simu na majirani. Ikiwa utakuwa na taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwa majambazi hao, unaweza kutoa taarifa katika kituo cha polisi ulicho karibu nacho

 

Comments

Popular posts from this blog