WAKUU WA SHIRIKA LA KUPAMBANA NA UFISADI NCHINI KENYA WASIMAMISHWA KAZI

Rais wa serikali ya Kenya, Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amewasimamisha kazi wakuu wawili wa shirika linalopambana na ufisadi nchini humo, siku moja tu baada ya bunge kupitisha mswaada inaowalaumu kwa uzembe na utepetevu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Ikulu ya Rais Manoah Esipisu, tume ya maadili na kupambana na ufisadi, itaendelea na kazi yake licha ya kusimamishwa kwa wakuu hao wawili.
Wakuu hao ambao ni Mwenyekiti, Mumo Matemu na naibu wake Bi. Irene Keino wamesimamishwa huku uchungunzi ukianzishwa dhidi yao kuhusiana na tuhuma za uzembe wa kazi na kutumia vibaya madaraka yao ikiwemo kujihusisha na ufisadi.
Tangazo hilo limetolewa mwezi mmoja baada ya ripoti kutoka ya tume hiyo kuwasilishwa kwa Rais Kenyatta, ripoti iliyosababisha kusimamishwa kazi kwa Mawaziri wanne wa serikali ya Uhuru Kenyatta na Maafisa wengine 12 na Wakuu serikalini ili kupisha uchunguzi ufanyike dhidi yao

Comments

Popular posts from this blog