KAMANDA MKUU WA BOKO HARAMU{ ABOU MOJAHID} AUAWA KIKATILI,


Askari wa jeshi la Nigeria
Msemaji wa jeshi la Nigeria Meja Jenerali Chris Olukolade amesema kuwa, vikosi vya nchi hiyo vimemuua kamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Boko Haram Abu Mojahid ambaye ameuawa katika mapigano kati ya jeshi la Nigeria na wapiganaji wa kundi hilo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Olukolade ameongeza kuwa, wapiganaji kadhaa wa Boko Haram nao wameuawa katika mapigano hayo.
Wakati huo taarifa kutoka Nigeria zinasema kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuukomboa msitu wa Sambisa ambao ulikuwa ngome ya mwisho ya kundi la kigaidi la Boko Haram.
Msitu wa Sambisa huko kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Hayo yanajiri ikiwa Operesheni ya pamoja ya vikosi vya Nigeria, Chad, Cameroon na Niger dhidi ya Boko Haram ikizidi kuendelea huku kukiwa na taarifa kwamba, imekuwa na mafanikio.

Comments

Popular posts from this blog