HAWAENDANI LAKINI NDO HIVYO TENA,SOMA HAPA

 
Aunt Ezekiel na Moze Iyobo.
NImtazamo wa wengi kuwa baadhi ya mastaa ambao wapo kwenye uhusiano hawaendani kabisa kutokana na muonekano wao, tabia zao na hata fani zao kuwa tofauti.
Kuna mastaa wa Bongo na wa Mamtoni ambao mapenzi yao yalivyoanza yaliwashtua watu mbalimbali na wengine kudai hayafiki mbali huku wale wanaotazamiwa kuendana kwa kila kitu wakimwagana vibaya mfano, Diamond Platnumz na Wema Sepetu, Rihanna na Chris Brown na wengineo wengi.
AUNT EZEKIEL NA MOSE IYOBO
Aunt Ezekiel ambaye ni staa wa Bongo Muvi alidai ‘kudate’ na dansa wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo, hiyo ilijulikana mwishoni mwa mwaka jana baada ya Aunt Ezekiel kudai kuwa mimba hiyo ni ya dansa huyo. Uhusiano huo uliwashtua mashabiki wengi wa staa huyo ambapo mpaka sasa hawakubaliani na uhusiano huo wakidai kuwa kuna mtu nyuma ya Mose ambaye ndiye muhusika wa mimba ya Aunt kwa kigezo kuwa Mose hana jeuri ya pesa ya kuweza kumuweka Aunt mjini.
.NAY WA MITEGO NA SHAMSA FORD
Huu ni moja tu ya mfano wa mapenzi yanayoendelea kutengeneza vichwa vya habari kwa sasa. Shamsa Ford ambaye ni staa wa filamu Bongo anatazamwa kama mtu mtaratibu, asiye na skendo wala majivuno huku Nay wa Mitego akitazamwa kama mtu mwenye majivuno, hasira na mkorofi. Mashabiki wa mastaa hao siyo kwamba wamepigwa na butwaa na uhusiano huo bali wanaendelea kuwafuatilia ili kujua nini kitatokea kwa kuwa wenyewe wanadai wana ‘projekti’ inayoendelea kati yao japo kuna picha wakiwa katika pozi za mahaba zinasema tofauti.

T.I NA TAMEKA
T.I ni rapa wa Marekani ambaye uhusiano wake na mkewe ulianza mwaka 2010 na hatimaye kuoana, uhusiano huo unatajwa kuwashangaza wengi kwa kuwa T.I anatazamwa kama mmoja wa marapa ‘handsome’ zaidi huku mkewe akipigwa vijembe kuwa ni mbaya. Lakini wenyewe hawajali hali hiyo na kuonesha mapenzi ya dhati ambapo mpaka sasa wana watoto wawili na siku zinasonga.

JAY-Z NA BEYONCE
Jay-Z ni rapa mwenye heshima kubwa nchini Marekani ambaye ni mume wa diva wa muziki wa Pop na R&B, Beyonce. Mwanzoni ilikuwa kama utani kuwa mtu kama Jay-Z angeingia kwenye uhusiano na Beyonce hadi kufikia kuoana.
Mitazamo ya watu kuwa Jay-Z ni mbaya kimuonekano na hawezi kuwa na mtoto mkali kama Beyonce ilikuwa ni chachu ya fikra hizo miongoni mwa watu. Mitazamo hiyo ikageuka vijembe ambavyo hata mastaa wenzake waliuzungumzia kiutani uhusiano wao, Lakini ndiyo hivyo tena, mapenzi ya Jay-Z na Beyonce kila siku yanazidi kwenda levo ny
 
TEMBELEA BLOG YETU KWA HABARI ZAIDI

Comments

Popular posts from this blog