EXCLUSIVE! KUMBE MUME WA BABY J AMEFUNGWA…

Baby J 1
Baby J ni miongoni mwa mastaa waliozaliwa mwezi wa tatu akiungana na mastaa wenzake  wakiwemo Bob Junior, Linah, Jokate, Menina, Peter Msechu na wengineo.Sasa hapa nakusogezea hii stori inayomuhusu msanii Baby J ambaye amefunguka kwenye Amplifaya ya Clouds FM kuhusiana na mume wake kufungwa pamoja na suprise ambayo hatoisahau katika maisha yake.…Baada ya kufanya suprise kubwa sana kwenye birthday yangu alipoamua kunivisha pete niliona kitu kubwa sana tofauti na vitu vingine, niliamini kweli hivi ni vitu nilivyokuwa naviwaza katika maisha yangu kwamba ipo siku mimi naweza nikawa mke wa mtu au nikapata mtu akanipenda kwa dhati, kwa hiyo kile kitu nilivyokiona pale nilikuwa nimefurahi sana na nilikuwa sijaamini…
Baby J 3
Millardayo:Kwa hiyo uliolewa…?
Baby J: “…Yes niliolewa lakini bahati mbaya siko naye baada ya kuoana maana yeye alikuwa anaishi Marekani lakini amepata matatizo, amekamatwa yuko mikononi mwa polisi hukohuko Marekani kwa kosa eti la madawa lakini sina uhakika..”
Baby J 2
Millardayo; “Umemfahamu kwa muda gan?…
Baby J; “…Sio kwa muda mrefu sana kwasababu mimi sikuwa wa kwanza kumfahamu bali  yeye alikuwa ananifahamu mimi kwasababu tu ya umaarufu wangu kwa hiyo haikuchukua muda sana kufahamiana naye, alikuwa Mtanzania lakini ambaye anaishi nje ya Tanzania kwa muda mrefu sana, amezaliwa Tanzania lakini hajakulia Tanzania…
Millardayo: “Toka amefungwa sasa hivi ni muda gani umepita…?”
Baby J: “…Sasa unatimia mwaka wa tatu, kitu kizuri au kikubwa kinachonipa nguvu kwamba yeye mwenyewe ananipenda ananiongelesha maneno mazuri sema bali ninakuwa na roho ya kibinadamu kwasababu najua mitihani kuna leo na kesho, amehukumiwa miaka saba…
baby j 4baby j 5
Millardayo: “ Unaweza kuvumilia miaka yote saba hiyo?…
Baby J: ‘…Na ndio maana awali nilikuambia kwamba mimi ni mwanadamu na hakuna mtu anayejua kuhusu kesho namwachia Mungu…
Millardayo:Kwa hiyo hapo ulipo wewe ni mke wa mtu…?”

Baby J : “… ndio ninayodhani mimi lakini kwa upande wa kidini yetu waislamu inasemakana sio mke wa mtu ila yeye hajanitamkia kitu chochote…

Comments

Popular posts from this blog