Chuchu Hans Afungukia madai ya kuachana na Mpenzi wake Vicent Kigosi ‘Ray’


Staa  wa Filamu Bongo, Chuchu Hans juzikati alifungukia madai ya kwamba ameachana na mchumba wake Vicent Kigosi ‘Ray’, akaeleza kuwa, hakuna ukweli wowote juu ya hilo.
 
Chuchu alifikia uamuzi wa kufafanua juu ya madai hayo juzi kufuatia tetesi zilizokuwa zimeenea kwamba yeye na kipenzi chake huyo wametibuana na sasa kila mtu kimpango wake.

Akifungukia juu ya uvumi huo Chuchu alisema: “Kutakuwa na watu wanaosambaza uongo huo, huwezi kuamini muda si mrefu nilikuwa na baby wangu Ray, tukawa tunashangaa tu juu ya umbeya huo.
 
“Nahisi watu wamechukulia kwamba tumeachana baada ya mimi kuamua kubadilisha jina nililokuwa nikilitumia kwenye akaunti yangu ya kwanza ya Instagram, nimetoa neno The Greatest na kubakiza jina langu, ilikuwa ni uamuzi tu.
 
“Siwezi kuachana na Ray na hata kama ikitokea tumeachana naamini kabisa Ray hawezi kurudiana na Johari wala Mainda, hao wanaosema eti kaniacha mimi karudiana na Johari wanachemka,” alisema Chuchu.

Comments

Popular posts from this blog