ZITAMBUE DALILI HATARI ZINAZOASHIRIA KWAMBA UHUSIANO WENU UMEFIKA UKINGONI



1. Kama mwenza wako hakupi kipaumbele katika mambo yanayotokea, pengine anaumwa lakini huambiwi chochote unakuja kusikia hayo kutoka kwa marafiki, anaandika kwenye mitandao ya kijamii, ama ndugu wengine! Anza kuchukua hatua.
2.Kama Wewe/mpenzi wako  anaandaa malengo bila kukushirikisha kuna dalili ya mahusionao yenu kuvunjika kwa sababu malengo ni kwaajili ya baadae na ukiona malengo yako hayamuhusu mwenza wako basi kuna shida.
3.Kama hamna furaha tena kama kipindi kile mlipokuwa mnaanza mapenzi yenu, kama hakuna tena utani na vitu vingine vinavyopelekea furaha baina yenu basi kuna hatari ya mahusiano yanakaribia kuvunjika

4.Unakuwa na furaha zaidi ukiwa na rafiki wa mpenzi wako mnapokuwa mnaongea, kucheza, utani nk kuliko mwenza wako. Au mpenzi wako anafuraha zaidi akiwa na marafiki zako kuliko wewe anza kuwa makini.

5.Kama wazo la kuendelea kuwa pamoja linaondoka kichwani kwako kutokana na sababu moja amanyingine kuna uwezekano wa mahusiano hayo kuelekea mwishoni.
6.Kama hakuna mawasiliano ya mara kwa mara mara nyingine siku kupita bila kuwasiliana na mpenzi wako bila sababu ya msingi, na  uwezo wa kuwasiliana upon a hakuna anayeshangaa jua hapo kuna tatizo. Kila mkiwasiliana ni Ugonvi tu! Kuna dalili za kuachana na mpenzi wako

7.Ukiona unahitaji kubadilika kutoka kwenye uhalisia uliokuwa nao mwanzo ili kumfanya mwenza wako kuwa furaha, ujue kuna jambo haliko sawa!

8.Kama utajikuta wewe ni mtu wa kusikitika na kulia kila siku kuhusiana na mahusiano yako basi jua uko katika mahusiano yasiyo sahihi. Kila mtu ana nafasi sawa ya kuwa na furaha duniani.

9. Mnakutana tu siku ya kujamiiana, au  hamfanyi tena mapenzi ukulinganisha na zamani  na mmeridhika na hilo, kuna dalili za kuachana.

10.Kama mwenza wako anaficha sana simu yake na hataki kabisa ushike, na Ukishika anakupa sababu ya dharula, ama pengine hamuaminiani kabisa! ujue kuna kitu kimejificha hapo!

MAONI NA USHAURI TUTEMBELEE KUPITIA Email:pharsnyanda@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog