KUNDI LA ISIS LAWACHINJA WAPIGANAJI WAKE ZAIDI YA 120 KWA KUJARIBU KUTOROKA

Wapiganaji wa ISIS wakiua kundi la watu kwa risasi©RT
Kundi hatari linalodai kutetea na kufuata haki za dini ya kiislamu linalopigana nchini Iraq na Syria la Islamic State limewanyonga wapiganaji wake wa kigeni zaidi ya120 kufuatia wapiganaji hao kutaka kuondoka na kurudi makwao na kuachana na kundi hilo.
Wapiganaji waliouwawa ni waliokuwa wakitumikia kundi hilo katika mji wa Raqqa nchini Syria walikamatwa wakijaribu kutoroka kurudi makwao kama chanzo cha taarifa hii kilipozungumza na mwandishi wa The Financial Times ambaye amedai watu wanaopinga vitendo vya ISIS na utawala wa Rais Bashar al-Assad amesema watu waliouwawa walikuwa wakijaribu kutoroka baada ya ISIS kutoa mwongozo mpya wa wapiganaji wake katika kuwazuia kukimbia.
Ingawa kuna wapiganaji wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaojiunga na kundi hilo kwakuhadaiwa kwamba ISIS itawasaidia kuielewa vyema dini ya kiislamu na mara baada ya kujiunga wanajikuta walidanganywa na matokeo yake wanajiingiza katika vitendo vya kikatili vya mauaji vinavyofanywa na wapiganaji wa kundi hilo na kutaka kujiondoka kitu ambacho hakiwezekani. Aidha taarifa hiyo inasema wapiganaji mara wanapojiunga hutakiwa kupigana na kutojitoa katika kundi hilo la linalodai kufuata misingi ya dini na kupokea vitisho kutoka kwa wapiganaji wengine wa ISIS kwamba watauwawa endapo watajaribu kutoroka.
Kumekuwa na kundi kubwa la vijana na watu wa makamo sehemu mbalimbali duniani ambao huadaiwa na kundi hilo la ISIS likiwashawishi kwa njia ya mtandao au kupitia wawakilishi wao waliopo nchi mbalimbali kwa kificho ili kwenda kujiunga nao katika mapigano ili kuendeleza ama kudumisha dini ya Kiislamu na matokeo yake hujikuta wamehadaiwa na kujiingiza kwenye mauaji yasiyo na hatia ya kuua hata watoto kwakisingizio cha dini, kitendo ambacho kimekuwa kikipingwa na waumini mbalimbali wa dini ya kiislamu na dini nyingine duniani.

Ni mauaji tu©21stcenturywire

Comments

Popular posts from this blog