WAZIRI MAKALLA ATOLEWA CHINI YA ULINZI WA POLISI BAADA YA MKUTANO WAKE KUFANYIWA VURUGU NA CHADEMA
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati), akiongozwa polisi kuingia
kwenye gari baada ya kutokea vurugu meza kuu, katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Kata ya Goba, Kinondoni Dar es Salaam, ambazo alidai
zilipangwa kwa makusudi na viongozi wa Chadema kwa lengo la kumvulugia
ziara yake ya kuwaelezea wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika
suala la upatikanaji wa maji ya uhakika jijini Dar es Salaam ifikapo
Septemba, mwakani.
PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Gari lililombeba Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, likilindwa na
polisi lililopokuwa linaondoka baada mkutano wa hadhara kuvunjika
kulikosababishwa na vurugu ambazo waziri alidai kuwa zilipangwa kwa
makusudi na wafuasi pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wakirumbana
na viongozi wa CCM, katika Kata ya Goba, Kinondoni, Dar es Salaam.
Makalla alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani.
polisi lililopokuwa linaondoka baada mkutano wa hadhara kuvunjika
kulikosababishwa na vurugu ambazo waziri alidai kuwa zilipangwa kwa
makusudi na wafuasi pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wakirumbana
na viongozi wa CCM, katika Kata ya Goba, Kinondoni, Dar es Salaam.
Makalla alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani.
Makalla akijadiliana na maofisa wa CCM na Polisi kabla ya kwenda kupanda gari na kuondoka.
Poilisi
wakiwadhibiti baadhi ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakisababisha
vurugu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Makongo. Kinondoni.
Polisi
wakimdhibiti mmoja wa viongozi wa Chadema wakati wa mzozo uliotokea
jukwaa kuu katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji, Makalla na wananchi
wa Kata ya Goba.
Kiongozi wa cHADEMA AKIZOZANA NA WA ccm jukwaani katika mkutano wa Makongo Juu.
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee akizoza jukwaani katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Goba na hatimaye kuvunjika
Polisi wakimdhibiti mfuasi wa Chadema asiendelee kufanya fujo katika mkutano wa Waziri na Wananchi wa Kata ya Goba
Askari
wa FFU, akilinda doria wakati waziri Makalla akikagua nyumba ambazo
watu wamejiunganishia isivyo halali eneo la Bonde la Msimbazi, Dar es
Salaam.
Makalla
na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (kushoto) wakiangalia pampu
zinazotumika kujazia maji kwenye malori yanayonyonywa kutoka kwenye
mabomba ya Dawasa. Pampu hizo zilinaswa uani mwa nyumba katika eneo la
Bonde la Mto Msimbazi Dar es Salam
Waziri
Makalla na viongozi wengini wakishanga kuona tanki kubwa la maji
lililojengwa chini ya moja kati ya nyumba tano katika eneo hilo ambazo
wamiliki wake wamejiunganishia maji ya Dawasa isivyo halali
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akimhoji mchezaji wa zamani wa
Simba, Dua Said ambaye alikuwa miongoni mwa watu watano waliokamatwa kwa
tuhuma za kujiunganishia maji isivyo halali kutoka kwenye mabomba ya
Mamlaka ya Maji Safi na Taka (Dawasa), kwenye nyumba zao zilizopo Bonde
la Mto Msimbazi, Kigogo, Dar es Salaam. Makalla alikuwa kwenye ziara ya
kukagua miradi ya maji Dar es Salaam
Askari wakilinda doria katika eneo hilo
Moja ya malori yanayojazwa maji katika eneo hilo. Nalo liko chini ya ulinzi
Waziri
Makalla akielezea athari zinazotokana na wizi huo wa maji ambapo
alisema kuwa katika nyumba hizo tano kila siku wanaiba maji lita laki
tatu, hivyo kila siku kuikoseasha serikali mapato ambapo kwa mwezi
yanafikia sh. bil 1.4.
Mbunge
wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akielezea jinsi atakavyoshirikiana na
Serikali katika mapambano dhidi ya ufisadi wa maji jijini na kwamba
atakuwa bega kwa bega kuhakikisha mswada wa adhabu kubwa kwa wezi wa
maji unapelekwa Bunge la Novemba mwaka huu.
Mchaezaji
wa zamani wa Simba, Dua Said akielezea kwa wanahabari na mbele ya
Waziri Makalla, jinsi anavyoshirikiana na Shirika la Maji Safi na Taka
Dar es Salaam (DAWASCO), katika biashara ya kuuza maji. Dua Said alikuwa
ni miongoni mwa watu watano waliokamatwa kwa tuhuma za kujiunganishia
maji ya Dawasco isivyo halali katika eneo la Bonde la Msimbazi
Bomba
jipya la maji likitandazwa eneo la Makongo tayari kwa maandalizi ya
kusafirisha maji kutoka Mtambo wa Ruvu Chini ambao upanuzi wake
umekamilika hivi karibuni.
Makalla
akiuliza swali kwa wakandarasi kuhusu utandazaji wa bomba hilo, wakati
wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dar na Pwani.
Waziri
Makalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mwenyekiti wa
CCM, Salum Madenge, (KUSHOTO) Deusdedit Mtiro (kulia) walipokuwa
wakimlaki alipowasili kwenye mkutano katika Kata ya Makongo.
WAFUASI WA CHADEMA WAKISHANGILIA NA KUMTAKA WAZIRI AWAHAKIKISHIE UPATIKANAJI WA MAJI MAKONGO JUU
Chadema na CCM wakishangilia katika mkutano huo
Waziri Makalla akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Makongo
Moja wa wananchi akilalamika mbele ya waziri kuhusu adha kubwa wanaipata ya maji eneo la Makongo juu
Msafara
wa viongozi wa Chadema na CCM ukielekea kwenye mkutano wa wananchi
katika Kata ya Goba ambao hata hivyo ulivunjika baada ya kutokea vurugu
WanaCCM wakimshangilia Waziri Makalla alipokuwa akihutubia wananchi katika Kata ya Makongo
Chadema wakishangilia wakati Halima Mdee akihutubia Makongo Juu
Mfuasi wa Chadema akilalama
Mdee akizungumza na wanahabari baada ya mkutano wa Kata ya Goba kuvunjika
Wana CCM WAKISEREBUKA
mNYIKA AKIZUNGUMZA NA WAFUASI WA cHADEMA BAADA YA MKUTANO KUVUNJIKA
Comments
Post a Comment